Akizungumza
na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la
kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu
wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho
na hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge
kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja.
Kabogo aliwataka wanachama wahitaji, wachukue kadi za ACT ili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu ,ikiwa ni jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbele kwa maslahi ya Taifa.
“Wananchi
nyie ni chachu ya chama kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti
wa serikali za mitaa kwa kukiamini na kukipatia ridhaa kiweze kuleta
mabadiliko
ya kimaendeleo” alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF
kigoma.
Kwa upande
wa Katibu ACT Kanda Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta
mabadiliko kwenye ulingo wa siasa,ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi
ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya
vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Katika ziara
hiyo ya uzinduzi wa matawi ya chama husika,ACT kimefanikiwa kufungua matawi
kwenye kata sita kati ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji,huku
baadhi ya viongozi kutoka UPD,CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hicho
kwa kudai wanahitaji
chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge.
Hata hivyo
wanachama 3500 wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi
la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia chama kipya cha Alliance For Change and
Transparency (ACT).
Habari Na:-
Magreth Magosso-Kigoma.





No comments:
Post a Comment