![]() |
|
Nyoka huyo
alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa na kumtoa nje ya maji na kisha
kumla.
|
![]() |
|
Baada ya mlo
huo mkubwa Nyoka alijiendea zake"lilikuwa jambo la ajabu sana, ''
|
![]() |
|
Chatu huyo
alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi wa QueensLand, kupigana
na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
|
![]() |
|
Nyoka
alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji na kisha kumla.
|
Chatu
ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana
na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo
lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera
na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili March 02,2014.
Nyoka huyo
mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye,
Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Tiffany
Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa
jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC.
"Tulimuona
Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya
miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano
lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya
maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada
ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,''
alisema Tifanny.
Bwana Corlis
alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka
Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema
mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine
aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili
walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.
''Sio kitu
unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
Source:-BBC-Swahili.









No comments:
Post a Comment