Taswira ya Basi la Yanga SC likipata ajali katika eneo la Mikese mkoani Morogoro hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 16, 2014

Taswira ya Basi la Yanga SC likipata ajali katika eneo la Mikese mkoani Morogoro hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa.


Basi la Yanga SC limepata ajali likitokea mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jana March 15,2014.


Basi hilo  lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali eneo na Mikese ,Mizani mkoani Morogoro baada ya Mabasi yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro.
Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi ,Leo March 16,2014, hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu imeondoka na usafiri wa basi jingine kuelekea jijini Dar es salaam.


Kikosi cha Young Africans kilichoanza  dhidi ya Mtibwa Sugar,: 1.Kaseja, 2. Juma Abdul, 3.Oscar, 4. Cannavaro, 5. Yondani, 6. Domayo, 7. Msuva, 8. Nizar/Dilunga, 9. Didier, 10. Okwi, 11. Kizza/Javu


Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar ,Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema



Benchi la Timu ya Soka ya Mtibwa ya Morogoro  Lilkiongzwa na Kocha wa Timu Hiyo  Meky Mexime Wa Kwanza Kushoto..



Mashabiki waliojitokeza kwa Wingi Katika Uwanja w Jamhuri Mkaoni Morogoro Jana march 15,2014, Katika Mchezo wa ligi kuu Kati ya Yanga Dhidi ya Mtibwa Sugar.

Aidha katika mchezo wao wa Ligi Hapo Jana March 15,2014 ,Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans ilitoka suluhu (0-0 ) dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar ya Manugu katika mchezo uiofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Huko Chamazi, Azam FC waliibamiza Coastal Union Bao 4-0 na kuendelea kujizatiti kileleni. Bao za Azam FC zilifungwa na Kipre Tchetche, Bao 2, John Bocco na Kevin Friday.

Azam FC wamecheza Mechi 19 na wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 43 na kufuata Yanga SC waliocheza Mechi 18 na wana Pointi 39.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad