|
Bw.Samuel Sitta ameshinda
nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba kwa kura 487 na Bw.Hashim Rungwe
kapata kura 69 huku walio piga kura
jumla ni Wabunge 566 ,kura zilizo halibika ni kura 7.
|
![]() |
|
Muonekano wa ukumbi wa bunge
ambako Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanakutana kujadili rasimu ya kanuni-Mjini
Dodoma,Tanzania.
|
Wajumbe wa
Bunge maalum la katiba wamemchagua Spika wa Bunge la 9 la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Bw Samuel Sitta kuwa Mwenyekiti wa bunge maalum la Katiba.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika leo jioni katika ukumbi wa Bunge hilo, Bw Sitta ambaye
pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikuwa akichuana na Bw Hashim
Rungwe ambaye aligombea Urais wa Tanzania mwaka 2010 kupitia NCCR Mageuzi kabla
ya kuhamia CHAUMA.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa uchaguzi huo, amesema Bw Sitta ameshinda
kiti hicho kwa kupata kura 487 ambapo Bw Hashim Rungwe amepata kura 69.
Aidha uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti utafanyika
kesho March 13,2014, jioni, ambapo kufuatia Mwenyekiti kutokea Tanzania bara,
Makamu Mwenyekiti atatakiwa kutokea Zanzbar kwa mujibu wa kanuni ambapo pia
suala la Jinsia litazingatiwa.








No comments:
Post a Comment