Mamlaka ya
Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha juu ya kuwapo kwa kimbunga kiitwacho Hellen
katika mwambao wa Bahari ya Hindi ambacho kitasababisha mvua kubwa inayozidi
mililita 50 ndani ya saa 24 kuanzia jana March 30,2014, katika mikoa 14 nchini.
Taarifa ya
mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana (March 30,2014) kwa vyombo vya habari imebainisha kuwa mvua
zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtara, Lindi, Tanga, Unguja, Pemba,
Singioda, Dodoma, Ruvuma, Katavi, Njombe, Mbeya na Morogoro.
Taarifa hiyo
imeongeza kuwa mvua hizo zilitarajia kuanzia jana na zitaendelea hadi Aprili
Mosi mwaka huu na wakazi wa mikoa hiyo, watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka
zinazohusika na maafa zimetakiwa kuchukua tahahadhari zinazotakiwa.
Imebainisha
kuwa, uwezekano wa mvua hizo ni asilimia 80 na ni mwendelezo wa mvua za masika
zinazoendelea kunyesha nchi nzima katika baadhi ya maeneo ambako hupata misimu
miwili ya mvua kwa mwaka.
“Mamlaka ya
Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa zaidi kadri
zitakavyopatikana,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa, uangalifu
na tahadhari vinahitajika ili kuepusha maafa zaidi.
Kimbunga
hicho kinakuja wakati baadhi ya maeneo nchini, wiki iliyopita zilikumbwa na
mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali sasa na
kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu.






No comments:
Post a Comment