![]() |
|
Bondia Mashali, akipozi na mikanda yake baada ya kukabidhiwa mkanda mmoja
Jana March 29,2014,Usiku baada ya kufanikiwa kutwaa taji la WBO uzito wa Light
kwa Pointi 97-93.
|
|
Mabondia Japhert Kaseba (Thomas Mashali) wakipambana wakati wa mpambano
wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa
Mashali. Mashali alishinda kwa Pointi.
|
Bondia
Thomas Mashali amefanikiwa kutwaa taji la WBO uzito wa Light Heavy baada ya
kumshinda kwa pointi Japhet Kaseba Jana March 29,2014,usiku kwenye ukumbi wa
PTA, Sabasaba, Temeke mjini Dar es Salaam.
Majaji wote watatu walimpa ushindi bondia wa Manzese wa pointi 97-93 dhidi ya mbabe wa Kinondoni baada ya pambano hilo la raundi la 10, ambalo lilimalizika bila mtu kuanguka chini hata kwa sekunde wala kuhesabiwa kwa kuleweshwa ngumi.
Kaseba
alifanya vizuri katika raundi ya saba na ya nane, lakini Mashali akazinduka
raundi ya tisa na kumalizia ya 10 pia vizuri.
Japokuwa hata
matokeo yangetangazwa sare kusingekuwa na malalamiko, lakini Japhet aliridhia
uamuzi wa majaji na kumkumbatia Mashali baada ya pambano.
Katika
mapambano ya utangulizi, Alan Kamote alimshinda kwa Technical Knockout (TKO)
raundi ya tano Karage Suba na kutwaa ubingwa wa UBO uzito wa Light, pambano
kati ya Freddy Sayuni na Rajab Maoja lilivunjika raundi ya nne baada ya Maoja
kuchanika na kushindwa kuendelea kugombea ubingwa wa PST.
Said Mundi alimpiga Jumanne Mohamed kwa pointi pambano la uzito wa bantam, Issa Nampepeche alimpiga kwa pointi Zuberi Kitandula uzito wa bantam pambano lisilo la ubingwa, Saidi Chaku alitoka sare na Jocky Hamisi pambano la Feather lisilo la ubingwa na Majid Said alimpiga kwa pointi Frank Zaga uzito wa bantam pambano lisilo la ubingwa pia.








No comments:
Post a Comment