Nyumba 20 zimeanguka katika tarafa za Kamachumu na Ibuga, wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 28, 2014

Nyumba 20 zimeanguka katika tarafa za Kamachumu na Ibuga, wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha.


Zaidi ya mashamba 100 ya migomba katika kijiji cha bulembo kata ya Ibuga wilayani Muleba mkoani Kagera,yamehalibiwa na mvua iliyonyesha leo March 28, 2014,ikiambatana na upepo mkali.


Ni nyumba mojawapo iliyoezuka paa na baadhi ya kuta kudondoka.

Moja ya nyumba zilizooezuka katika kijiji cha bulembo kata ya Ibuga wilayani Muleba mkoani Kagera, leo March 28, 2014,kufuatia mvua iliyoambatana na  upepo mkali kunyesha.

Aidha kufuatia mvua hiyo ,Pia nyumba 15 zimeezuliwa na upepo katika kisiwa cha Musira kilichoko Manispaa ya Bukoba.

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa kisiwa hicho Bw. CHALES POLEPOLE amesema  kuwa pamoja na kuezuliwa kwa nyumba hizo pia mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba huku miti na migomba ikiharibiwa vibaya kutokana na upepo huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad