![]() |
|
Mtoto Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada
ya kupata ajali ya Moto akiwa na mama
yake Mzazi.
|
|
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo.
|
Mtoto Adolotea
Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze
kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Akizungumza kwa
masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa
Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata
janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo
Mtoto huyo aliungua vibaya.
Anasema tukio hilo
lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha
afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya
kula na kufurahi na wenzake.
Anasema tangu kipindi
hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu
baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe
ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze
kutibiwa.
Ameongeza kuwa baada
ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza
kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika
na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT
Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
Aidha kutokana na
kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze
kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza
kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.
Amesema anahitaji
zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu
pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati
akisubiri matibabu ya Mwanaye.
Mtu yeyote mwenye
kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia
simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini
Mbeya.
Na Mbeya yetu








No comments:
Post a Comment