Manchester City chini ya Meneja Manuel Pellegrini, wametwaa Taji lao la kwanza la CAPITAL ONE CUP baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 03, 2014

Manchester City chini ya Meneja Manuel Pellegrini, wametwaa Taji lao la kwanza la CAPITAL ONE CUP baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1.


Manchester City wakishangilia kwa furaha wakiwa  chini ya Meneja Manuel Pellegrini, jana Marchi 02,2014, Uwanja wa Wembley Jijini London wametwaa Taji lao la kwanza baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1 kwenye mchezo wa fainali na kubeba CAPITAL ONE CUP ambalo ndio Kombe la Ligi Nchini Uingereza.

Mchezaji Samir Nasri akishangilia baada ya kufunga bao la Pili huku goli  la kwanza la City lilifungwa na Yaya Toure kwa kigongo cha Mita 30 na Bao la Tatu la City ilifungwa na Jesus Navas alieingizwa Dakika ya 58 kumbadili Sergio Aguero.
Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea Uwanja wa Wembley Jijini London wakitwaa Taji lao la kwanza baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1 na kubeba CAPITAL ONE CUP  ambapo katika mchezo huo wa Fainali Jana March 02,2014,Sunderland walianza vyema kwa kufunga Bao katika Dakika ya 10 Mfungaji akiwa Fabio Borini lakini City walizinduka Kipindi cha Pili na kupiga Bao 3.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad