 |
Chumba cha
blog hii kupitia Whatsapp , kimearifiwa na kutumiwa picha za tukio la ajali eneo la Daraja la mto
Ruvu barabara kuu ya Dar es salaam-Morogoro na Mdau Elisante, akitufahamisha kutokea kwa Ajali ya Basi la Taqwa leo Asubuhi,
lililokuwa limetoka Leo March 18, 2014,Dar es salaam kupita wilayani Ngara
mkoani Kagera, kesho March 19, 2014,Asubuhi kwenda Jijini Bujumbura nchini
Burundi kupata ajali ambapo katika tukio hilo abiria kadhaa wamejeruhiwa.
|
Kulingana na
mashuhuda wa tukio hilo, wamebainisha kuwa athari ya ajali hiyo imesababishwa
na basi lingine kulipita basi la taqwa ,kisha likiwa mwendo kasi kukutana na
magari mengine mbele yake, hivyo Dereva wa basi la Taqwa kutaka kutanua zaidi ndipo
lilipomshinda na kupinduka.
Blog ya
Mwanawamakonda tunatoa pole kwa Majeruhi na tunawaombea wapone haraka majeraha
yao’’AMINA.
No comments:
Post a Comment