Uyoga ni
miongoni mwa vyakula adimu sana duniani. Lakini ni miongoni mwa vyakula vyanye
virutubisho muhimu sana kiafya tofauti na watu wengi wanavyodani.
Kwa mujibu
wa mtandao wa www.organicfacts.net uyoga una vitamini na aina nyingi za
madini.Baadhi ya virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja
na Vitamini B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na ‘Phosphorus’.
Wataalamu
hao wanaeleza kuwa virutubishoi vilivyomo ndani ya uyoga kuwa vina uwezo mkubwa
sio tu wa kuimarisha kinga mwilini bali pia kupambana na maradhi.
Mtandao huo
pia umeendelea kueleza kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri cha madini ya chuma
na shaba yanayohusika katika uwezeshaji wa usambaza wa hewa ya oksijeni
mwilini.
Vitamini B2
inayopatikana kwenye uyoga, ni tiba kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa
kichwa unaojulikana kama ‘kipanda uso’.
Kwa kula
kiasi kidogo cha mmea huo utajiweka kwenye nafasi ya kuwa na hali nzuri
hususani kwa wale wagonjwa wa kipanda uso.
Vitamini B
kwenye uyoga, ina uwezo wa kuzuia uchovu wa mwili na akili hasa wakati wa kazi
nyingi. Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini, wakati
Vitamini B6 huondoa hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au shambulio la moyo.
Pia, una
madini ya zinki yanayoimarisha kinga ya mwili pia husaidia kuponya haraka
vidonda si hivyo tu faida nyingine husaidia ukuaji mzuri wa seli za mwili,
huimarisha kiwango cha sukari mwilini na kukufanya usikie ladha , harufu ya
vyakula na vitu vingine ipasavyo.
Source:-Mwananchi.






No comments:
Post a Comment