Kura hizo
zimetangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge ,hilo, Mhe.Samia Sululu kabla
ya kuahirisha kikao hicho leo usiku, ambapo alisema
azimio hilo limepitishwa na Bunge hilo , kufuatia upigaji wa
kura ,ambapo idadi ya kura zilizopigwa ni 509, wakati
mauhudhurio ya wajumbe yalikuwa 511.
Mhe . Samia
alisema kwa upande wa kura za wazi zilizopigwa ni 438, ambazo za ndiyo
zilikuwa 351 na hapana ni 87, wakati kura za siri zilizopigwa zilikuwa ni
71, ambazo za ndiyo zilikuwa 25 na hapana ni 46.
Uamuzi huo
umefuatiwa baada ya hali hiyo ambayo ilitokea tena kwa mara nyingine
jana jioni mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge
Maalum, Mhe . Kificho kuwasilisha mapendekezo ya upigaji kura wa wazi na
siri kutumika kwa pamoja katika kaununi hizo.
Tangu jana
jioni na leo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakitoa michango kutaka upigaji
kura huo uwe wa wazi na siri , huku wengine kutaka kura ya siri.
Awali
Kanuni za 37 na 38 zilibaki kiporo tangu wakati wa utungaji wa
kanuni mbalimbali za Bunge hilo, na uchangiaji wa
kuziboresha, kutokana na mvutano huo, ambao baadhi ya wajumbe kutaka kura
ya uwazi na wengine siri.
Wakizungumzia
juu ya makubaliano yaliyofanywa na Kamati ndogo ya Muda ya Maridhiano na
Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge kuhusu mapendekezo ya upigaji
kura huo.
Mmoja ya wajumbe
wa Kamati hiyo ndogo ya Maridhiano, John Nyika alisema walifanya
mazungumzo hayo waliona ni vema wakubaliana mtu anayeweza
kupiga kura ya uwazi na anayetaka ya siri wapige kulingana na matakwa yao
ili kuwezesha mchakato huo kupiga hatua mbele.
“ Tunaomba
utaratibu huu wa maridhiano uendelee … ili tuweze kupiga
hatua mbele,” huku akisisitiza hawana dhamira yoyote ya kukwamisha
mchakato wa Katiba mpya. Hivyo watakuwa wa kwanza kuunga mkono kwa kura azimio
litakalopitishwa kwa kura zitakazokubaliwa.
Naye mjumbe
mwingine wa kamati hiyo , Vuai Ali Vuai alisema jambo hilo ni kubwa kwa
Watanzania ndio maana wanatakiwa kupiga kura kwa uwazi umma uweze kuona .
Kwa
upande wake ,mjumbe mwingine wa kamati hiyo ya ndogo ya Maridhiano Askofu
Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela
amesema ni vizuri wajumbe hao wakakubali azimio hilo kwa kuwa mpaka
sasa wameshatumia siku 40 kujadili kanuni za kuongoza Bunge hilo na zimetumia
gharama hivyo wasiendelee kuongeza gharama, zipo siku tatu za kuomba ili
kufanikisha maridhiano hayo.
“ Ninawaomba
wajumbe wenzangu kukubali azimio hili ili tuweze kusonga mbele na na mchakato
wa kupata Katiba ,” alisema Askofu Mtetemela.
MATOKEO YA KURA BUNGENI :-
1. KURA ZA WAZI ZIMEPIGWA JUMLA 438.
A. KURA ZA WAZI ZILIKUWA HIVI:- (1). NDIO 351 (2). HAPANA 87
2. KURA ZA SIRI:- (1). HAPANA 46 (2). NDIO 26.
2. KURA ZA JUMLA ZA HAPANA:- (1). 133 (2). NDIO 376.
- KANUNI YA WANAOTAKA KUPIGA KWA SIRI NA WAZI IMEKUBALIKA RASMI.






No comments:
Post a Comment