ATHARI :- Mvua inapoleta adha kubwa Jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 29, 2014

ATHARI :- Mvua inapoleta adha kubwa Jijini Dar es Salaam.


Roli likiwa limekatiza barabara baada ya kushindwa kupandisha mlima na kuteleza hadi kuingia mtaroni pembezoni mwa barabara ya Goba kutokea Mbezi Luisi, karibu na Mbezo Luxy, kutokana na utelezi wa mvua iliyonyesha March 28, 2014.

Daraja la Mtama linalounganisha barabara kati ya Lindi na Newala likiwa limekatika jana kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Picha hii na Ahmed Abdulaziz. 

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimeleta adha kubwa, huku baadhi ya wakazi wakilazimika kuhama baada ya makazi yao kukumbwa na mafuriko.

Aisha sehemu mbalimbali jijini March 28,2014,zilikumbwa na mafuriko makubwa, huku baadhi ya nyumba kuta zake zikiwa chini baada ya kuzidiwa na maji.

Hapa ni eneo la millenium tower makumbusho, mvua kubwa ilioyensha March 28,2014 na Asubuhi imepelekea kuwepo kwa maji mengi eneo hili hadi kupelekea magari yaendayo posta kupitia pakinng ya magari ya eneo hili au ya jengo hili la millenium tower  na kusababisha msongamano wa magari na hata Bar  za pembezoni mwa sehemu hiyo na Grosari zote zililazimika kufungwa kwa muda sambamba na Maduka kutokana na maji mengi kuingia sehemu zao za biashara. 
Wakazi wa Jangwani karibu na uwanja wa klabu ya Yanga wakiwa wamekaa juu ya paa la nyumba kukwepa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea nchini.
Muonekano wa nyumba pamoja na njia ndogo ndogo zikiwa zimejaa maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad