![]() |
|
Lionel Messi
akishangilia baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa Barcelona wa 1-0
dhidi ya jirani zao Espanyol.
|
Mshambuliaji
Messi amevunja mwiko wa kutowafunga Espanyol kwenye Uwanja wao wa Cornella El
Prat baada ya Jana March 29,2014, kuifungia bao pekee FC Barcelona dhidi ya
wenyeji wao hao.
Messi
hakuwahi kufunga katika Uwanja huo katika misimu mitano, lakini jana hakufanya
makosa alipokwenda kupiga penalti baada ya beki wa pembeni, Javi Lopez kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari.
Barcelona
sasa inafikisha pointi 75 baada ya mechi 31 na inaendelea kukaa nafasi ya pili
nyuma ya Atletico Madrid yenye pointi moja zaidi, baada kuifunga Athletic Club
2-1.
![]() |
|
Cristiano
Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real bao lake la 28 katika msimu huu wa
La Liga.
|
Nae nyota wa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walirejesha urafiki wao tena
wakati timu yao ikiifumua mabao 5-0 Rayo Vallecano Jana March 29,2014,usiku katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa
Santiago Bernabeu.
Bale alimsetia
Ronaldo kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 14, na akachangia bao la
pili lililofungwa na Carvajal dakika ya 54, kabla ya kufunga la tatu dakika ya
67 na la nne dakika ya 70 wakati Morata alifunga la tano dakika ya 77.
Real sasa
inatimiza pointi 73 baada ya mechi 31, lakini inaendelea kuketi nafasi ya tatu
nyuma ya FC Barcelona yenye pointi 75 na Atletico Madrid pointi 76 kileleni,
zote zikiwa zimecheza mechi 31 pia.
Ronaldo
alimkasirikia Bale baada ya kwenda kupiga mpira wa ovyo dakika za mwishoni Real
ikilala 4-3 mbele ya Barcelona wiki iliyopita, lakini jana amemaliza hasira za
mchezaji mwenzake huyo na kurudisha urafiki wao tena.
| Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Atlético Madrid | 31 | 47 | 76 |
| 2 | Barcelona | 31 | 64 | 75 |
| 3 | Real Madrid | 31 | 54 | 73 |
| 4 | Athletic Bilbao | 31 | 19 | 56 |
| 5 | Sevilla | 31 | 9 | 50 |
| 6 | Real Sociedad | 30 | 10 | 49 |
| 7 | Villarreal | 30 | 14 | 48 |
| 8 | Espanyol | 31 | -2 | 40 |
| 9 | Valencia CF | 30 | 1 | 40 |
| 10 | Levante | 30 | -11 | 37 |
| 11 | Celta de Vigo | 31 | -10 | 36 |
| 12 | Granada CF | 30 | -12 | 34 |
| 13 | Rayo Vallecano | 31 | -34 | 33 |
| 14 | Málaga | 30 | -9 | 32 |
| 15 | Elche | 30 | -17 | 31 |
| 16 | AlmerÃa | 30 | -24 | 30 |
| 17 | Osasuna | 30 | -26 | 29 |
| 18 | Getafe | 30 | -21 | 28 |
| 19 | Real Valladolid | 30 | -19 | 27 |
| 20 | Real Betis | 30 | -33 | 22 |







No comments:
Post a Comment