EPL 2013/2014:-Ripoti ya Mechi Ligi kuu Uingereza huku Chelsea ikilichwa ugenini na Matumaini yake ya Ubingwa kuingia Dosari. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 29, 2014

EPL 2013/2014:-Ripoti ya Mechi Ligi kuu Uingereza huku Chelsea ikilichwa ugenini na Matumaini yake ya Ubingwa kuingia Dosari.


Nahodha wa Chelsea, John Terry akipiga kichwa kutumbukiza mpira kwenye lango la kipa wake, Petr Cech na kupoteza Matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza 2013/2014 baada ya kuchapwa Bao 1-0 na Crystal Palace katika mchezo huo wa Ligi uliochezwa Leo March 29,2014.


Mchezaji wa Crystal Palace, Jason Puncheon (kushoto) akishangilia huku Terry akisigina kichwa chake chini baada ya kujifunga na kuipa ushindi wa bao 1-0 Crystal Palace.

Wachezaji wa Crystal Palace wakishangilia ushindi wao wa leo dhidi ya Chelsea.

Matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza yameingia dosari kubwa leo March 29,2014,baada kuchapwa Bao 1-0 na Crystal Palace, Timu ambayo inapigana kujinusuru na kubakia kwenye Ligi hiyo, katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Selhurst Park.

Bao hilo la ushindi kwa Palace lilifungwa na Nahodha wa Chelsea, John Terry, baada kupiga Kichwa wavuni kwao wenyewe kufuatia Krosi ya Dakika ya 52 ya Joel Ward.
Mara mbili Kipa wa Palace, Julian Speroni, aliokoa toka kwa Eden Hazrd na pia John Terry alipata nafasi safi lakini Kichwa chake kilipaa.

Palace walikaribia kupata Bao la Pili lakini Shuti la Cameron Jerome lilipiga Posti.

Huo ni mchezo wa pili mfululizo The Blues wanafungwa ugenini, baada ya awali kufungwa na Aston Villa na sasa inabaki na pointi zake 69 za mechi 32 mbele ya Liverpool yenye 68 za moja 31.


Rooney akifunga kwa penati na kuipa Mabao mawili Manchester United katika dakika za 20 na 45 na mengine ya Juan Mata dakika ya 57 na Javier Hernandez dakika ya 90 yalitosha kuiongezea pointi United.

Juan Mata akipambana na Bacuna  na furaha kwa kocha David Moyes kufuatia Manchester United kuifunga mabao 4-1 Aston Villa Uwanja wa Old Trafford March 29, 2014,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza. 

Mabingwa wa Uingereza, Manchester United, wakicheza kwao Old Trafford Leo  March 29, 2014, wamepata Mechi nzuri ya kupasha moto kabla Jumanne hawajawavaa Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI itakayochezwa Uwanjani hapo hapo baada ya kuitandika Aston Villa Bao 4-1 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.

Aston Villa ndio waliotangulia kupata Bao kati Dakika ya 13 baada ya Frikiki ya Westwood kumshinda nguvu Kipa De Gea lakini Wayne Rooney akaifungia Man United Bao 2 moja likiwa Penati iliyotolewa baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya Boksi.

Juan Mata aliongeza Bao la Tatu katika Kipindi cha Pili na hilo ni Bao lake la Kwanza tangu ahamie Man United Mwezi Januari kutoka Chelsea.

Bao la 4 lilifungwa na Chicharito, alietokea Benchi, baada ya kazi nzuri ya Adnan Januzaj ambae nae pia aliingizwa Kipindi cha Pili.

Kabla Mechi hii kuanza Washabiki wa Manchester United walionyesha sapoti yao kwa Meneja wao David Moyes kwa kumshangilia wakati akiingia Uwanjani kwenda kukaa kwenye Benchi kabla Mechi kuanza na kuizomeoa ile Ndege iliyopita juu ya Anga ya Old Trafford ikiburuza Bango kubwa: 'Wrong One - Moyes Out' wakati Mechi imeanza tu.
Mashabiki, hasa wale waliokwaa Jukwaa maarufu la Old Trafford liitwalo Stretford End, waliimba na kumshangilia Moyes: “One David Moyes!”.

MATOKEO YA MECHI  LIGI KUU UINGEREZA.

Man Utd 4 - 1 Aston Villa
Crystal Palace 1 - 0 Chelsea
Southampton 4 - 0 Newcastle
Stoke 1 - 0 Hull
Swansea 3 - 0 Norwich
West Brom 3 - 3 Cardiff  
Arsenal 1 - 1 Man City 

RATIBA LIGI KUU UINGEREZA.


Jumapili Machi 30,2014.

1530 Fulham v Everton
1800 Liverpool v Tottenham

Jumatatu Machi 31,2014.

2200 Sunderland v West Ham
 

Position Team Played Goal Difference Points
1 Chelsea 32 38 69
2 Liverpool 31 45 68
3 Man City 30 52 67
4 Arsenal 32 19 64
5 Everton 30 16 57
6 Tottenham 31 0 56
7 Man Utd 32 14 54
8 Southampton 32 9 48
9 Newcastle 32 -9 46
10 Stoke 32 -8 40
11 West Ham 31 -7 34
12 Aston Villa 31 -12 34
13 Swansea 32 -3 33
14 Hull 32 -7 33
15 Norwich 32 -25 32
16 Crystal Palace 31 -19 31
17 West Brom 31 -12 29
18 Cardiff 32 -32 26
19 Sunderland 29 -19 25
20 Fulham 31 -40 24

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad