Kituo kipya cha Redio kuanza kurusha matangazo Bukoba ni kupitia 93.3Mhz. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 01, 2014

Kituo kipya cha Redio kuanza kurusha matangazo Bukoba ni kupitia 93.3Mhz.


Kituo kipya cha redio kitaanza kurusha matangazo yake hivi karibuni katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ,baada ya serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano (TCRA) kutoa kibali cha kudumu kwa shirika la maendeleo na kundoa umaskini KADETFU kukubaliwa kuendesha redio hiyo.
Katika Mahojiano maalum na Harakatinews  Mkurugenzi wa Kadetfu Bw Yusto Muchuruza (pichani chini) amesema kuwa rediyo hiyo iitwayo  Kagera Community Radio ( KCR FM  itarusha matangazo kupitia masafa ya 93.3MHz .

Kwamba, Wazo la kuanzishwa kwa redio hii ilikuwa ni pamoja na kutaka kubadili maisha ya jamii  katika nyanja mbalimbali hasa  kujenga uelewa juu ya masuala ya msingi ya jamii kama vile jinsia, ulinzi wa mazingira, haki nyingine za kijamii na kiuchumi,tatizo la VVU / UKIMWI  na  kupunguza umaskini miongoni mwa mengine.

Hivi sasa uongozi wa KADETFU upo katika harakati za ujenzi wa studio,minara na taratibu za mwisho mwisho kabla ya kuanza matangazo rasmi. 

Redio nyingine zinazorusha matangazo yake kutoka Mkoani Kagera ni Redio Kwizera FM( wilayani Ngara),Redio Karagwe na Redio Fadeco (wilayani Karagwe) pamoja na Redio Vision na Kasibante FM za Manispaa ya Bukoba.

Kama Unataka ufafanuzi zaidi juu ya redio hiyo GONGA HAPA.

Source:- Harakatinews

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad