Soma utafiti huu ni muhimu kwako:-Leo ni siku mbaya kwa wenye wapenzi wa ovyo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 14, 2014

Soma utafiti huu ni muhimu kwako:-Leo ni siku mbaya kwa wenye wapenzi wa ovyo.



Leo feb 14,2014,ni Siku ya Wapendanao ‘Valentine Day’. Lengo hasa la siku hii ni kuonyesha upendo kwa watu au mtu ambaye unampenda kwa dhati…. Kwa wale ambao hawana wapenzi waaminifu, ni siku ya kilio na kutokuwa na furaha. Pole sana wewe ndugu yangu usiye na mpenzi bora, leo ni siku ya presha.
Kwa wale ambao hawana wapenzi waaminifu, ni siku ya kilio na kutokuwa na furaha. Pole sana wewe ndugu yangu usiye na mpenzi bora, leo ni siku ya presha.

Kama una mwenza ambaye ni wa ovyo kwa maana kwamba siyo mwaminifu, leo huenda ikawa ni siku mbaya kwako, atakukera kwa namna tofauti hasa kutopenda kuwa karibu. Baadhi ya watu leo simu zitakuwa na matatizo hasa kuisha chaji au mawasiliano (netiweki) kutokuwa nzuri.

Ushauri wangu ni kwamba kama una mwenza asiyetulia, itakuwa ni makosa makubwa kukubali kuoana naye; usikubali hata siku moja kuoana na mtu ambaye kabla ya ndoa anaonekana kuwa na wapenzi wengi.

Ni maumivu juu ya maumivu.

Ni kutokana na ukweli kuwa wengi wa watu wanaopendana kwa dhati au wanaopenda kuchezeana, leo huwa wanapenda kuwa pamoja, kama mwenzi wako ana wapenzi wengi, leo hawezi kukupa raha. Kama hamko karibu, hata simu yake kuna wakati haitapatikana au haitapokelewa au haitapokelewa kwa wakati, tofauti na ulivyomzoea. 

Wapo ambao watarudi wamechoka hoi...kishachoshwa huko nje! Ingawa lengo la siku hii siyo kuendekeza ngono  au uzinzi kama nilivyosema, wapo watu wengi furaha yao ni kuendekeza ngono.

Nini cha kufanya katika siku ya leo.

Jambo la msingi ni kwa kila mtu kuwa na upendo wa dhati kwa mwenzi wake. 

Ni ujinga kuendekeza ngono au uzinzi...wapo ambao wameshafanya sana na wanawake au wanaume wengi, hakuna walichopata zaidi ya kuwa na hofu kwamba ‘sijui nimeambukizwa ugonjwa nk’.

Kila mwenye akili timamu anapaswa kutafakari sana, kwani ukweli ni kwamba tabia hizi hazina maana katika maisha yetu. 

Leo iwe ni siku ya watu kufurahiana, siyo kutesana mioyo kwa kuonyeshana kwamba wewe una uwezo wa kuwa na wanawake au wanaume wengi kama ambavyo baadhi ya watu wanafanya. 

Kwa wale ambao hawako kwenye ndoa, ni vizuri kuwa makini sana katika kuchagua mwenza, chagua mtu ambaye anaushibisha moyo wako ili hata baadaye usiwe mwenye kuhangaika na wanaume au wanawake wengine nje ya ndoa.

Utajuaje ana mwingine?

Kuna namna nyingi za kujua, lakini mojawapo ya dalili kwamba huenda asiwe mwaminifu ni kwamba hawi wazi katika suala la mawasiliano, kama ni simu huwa inafungwa kwa namba za siri au kupokea kwa kificho; kwa jumla anakuwa mwenye hofu na namna anavyoitumia simu yake.

Anaweza kudanganya kwa kutaja sababu nyingi, lakini wengi wa watu ambao si waaminifu, hawana amani na simu zao. Wengine ukiwa naye anazima ili asipigiwe na mwingine au wengine alionao. Wengine leo huanzisha safari au namna yoyote ili uwe mbali naye.

Hata hivyo ni rahisi mno kujua kama mwanamke ametoka au la, kwa mfano angalia namna anavyojipendezesha anavyotaka, je, zamani alikuwaje na sasa yukoje? Je, akitoka mkiwasiliana mawasiliano yanakuwaje? Kwa wanawake pia kama hajakutana na mwanamume muda mrefu hutoa aina fulani ya uchafu mweupe, au huwa uko ndani sana na hauwezi kuondolewa kwa namna yoyote zaidi ya tendo la ndoa. Unamjua mwenzi wako, mabadiliko ya tabia yanapotokea, pata kuangalia sababu ni nini, chukua hatua.
  
Na:-Dismas Lyassa/Kwa maoni/Ushauri 0688487745

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad