Kuna mambo mengi yamezungumzwa tangu jana na hadi leo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa marudio katika kata 27 na ushindi wa CHADEMA katika kata 3 za Kiborloni, Sombetini na Njombe mjini. |
Moja ya
masuala yanayozungumzwa na wapinzani wa CHADEMA, ambayo hata leo katika press
conference iliyoitishwa Lumumba, litazungumza sana, ni kujaribu 'kuoanisha'
M4C-OPD (matumizi ya chopa 3) na ushindi wa kata 3.
Kuoanisha
mambo hayo kwa mgongo wa kufanya uchambuzi au tathmini ya mambo hayo mawili, ni
ama kuamua kuwa myopic kwenye hoja muhimu au kuamua kupotosha kwa makusudi ya
propaganda nyepesi au kutokujua tu.
Wakati
Mwenyekiti Mbowe anazindua M4C- Operesehni Pamoja Daima, mbele ya waandishi wa
habari alisema malengo ya shughuli hiyo maalum kuwa itaweka msisitizo au mkazo
kwenye masuala makuu yafuatayo;
Kwa wale
waliofuatilia OPD, kila mtu anajua namna ambavyo imeibua mjadala mkali katika
masuala hayo, kuanzia na katiba mpya, wazawa na matumizi (unufaikaji) ya
rasilimali, ugumu...
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ikalazimika kutangaza kwamba tayari serikali imetoa fedha za
kuboresha daftari la wapiga kura. Haitoshi tu kusema hivyo. Viongozi wakuu,
Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa wakatoa kauli ya chama wakiitaka NEC
itoe taarifa kamili juu ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na;
Ratiba kamili ya shughuli hiyo Lini NEC
itaanza kukagua vituo Tarehe rasmi ya kuanza kuboreshwa daftari Serikali imetoa
bajeti ya kiasi gani (inatosha kwa shughuli nyeti kama hiyo?
Kwa sababu
M4C-OPD ilikuwa ni ya nchi nzima, yako maeneo ya uchaguzi ambako chopa
zilifika.
Lakini kuoanisha matumizi ya chopper 3 na matokeo ya ushindi wa kata
3, ni kulazimisha hoja isiyokuwepo kwa premises za kuokoteza Wapinzani wa
CHADEMA wakisukumwa na euphoria ya ushindi usiokuwa na uhalali (tutafafanua),
wamejikita kwenye 'negative (ya picha)' inayozungumzia chopper 3 kwa kata 3,
wanashindwa kuiona 'picha kubwa' (negative Vs bigger picture), inayozungumzia
masuala kadhaa, mfano;
Katika
uchaguzi wa 2010 matokeo yalikuwaje?
Je kuna
mabadiliko ya goal post, figures na namba?
Je
mabadiliko hayo yako in favour of status quo au yanasapoti vuguvugu la
mabadiliko?
CHADEMA
itajikita katika hayo kwa sababu ni muhimu sana katika suala kulinda demokrasia
ya watu na kusheherekea ushindi, hasa ushindi ulio halali.
Mfano;
katika Kata ya Njombe mjini, mwaka 2010 CHADEMA haikusimamisha mgombea kabisa
wa udiwani wala ubunge. Mgombea Urais wa CHADEMA alimzidi kwa mbali mno mgombea
urais wa CCM. Mbali mno.
Matokeo ya
jana katika kata hiyo hiyo kwa uchaguzi wa udiwani, yanaonesha kwamba;
CHADEMA
imepata kura 2,202 CCM imepata kura 1,094
Jumla ya
kura zilikuwa 3334
Jumla ya
vituo vilikuwa 41, CCM imeshinda kituo kimoja tu kwa tofauti ya kura 9
Iko mifano
mingi ya namna hii katika uchaguzi wa jana. Kuna maeneo ambayo CHADEMA
haikuwahi kuweka mgombea, imetoa ushindani mkali na kuna maeneo ambayo uchaguzi
uliopita kulikuwa na tofauti kubwa mno ya kura, lakini safari hii gap
limepunguzwa kwa namba kubwa sana.
Mfano Kata
ya Mpwayungu, Mtera, Dodoma Mwaka 2010
CHADEMA 602
CCM 1812
Mwaka 2014
(jana)
CHADEMA 555
CCM 872
Katika Kata
ya Ubagwe, mwaka 2010, CCM ilipita bila kupingwa. Uchaguzi wa jana umekuwa;
CCM 329
CHADEMA 215
TADEA 71
Zilizoharibika
3
Where are
the voters? Where is legitimacy?
Moja ya
masuala ya msingi sana ambayo tulitarajia yawaumize kichwa sana watu, hususan
walioko madarakani ni swali hili; Je wapiga kura wako wapi?
Suala hili
limepewa uzito na CHADEMA pamoja na wapenda demokrasia na maendeleo wengine
wengi tu nchini tangu baada tu ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Nani
anajali?
Walioko
madarakani wangelikuwa wanathamini mchakato wa demokrasia ya uwakilishi, ambayo
maana yake ni kuwaheshimu watu/wapiga kura, kamwe wasingekuwa wanakimbilia
kushangilia matokeo, tena yasiyowapatia uhalali.
Mathalani
Kata ya
Ubagwe, Ushetu, Shinyanga,Wapiga kura
walioandikishwa wako 4270
Waliopiga
kura jana ni 618
CCM
wameshinda kwa kura 329 dhidi ya CHADEMA kura 215, TADEA- 7, zilizoharibika 3.
Kata ya
Nyasura Bunda,
Waliojiandikisha
ni 5333
Waliopiga
kura 1579
Wapiga kura
wako wapi? Uko wapi uhalali wa ushindi wa kata nyingi?Aidha, wapinzani wa
CHADEMA hawataki kabisa kabisa kuzungumzia irregularities.
Very serious
irregularities done purposefully. Hawataki kabisa kugusia namna ambavyo watu
wamepigwa wazi wazi na kuchukuliwa kwenye vituo vya kura, wakiwemo mawakala wa
CHADEMA kisha eti wakapelekwa vituo vya polisi.
Wapenda
demokrasia hao ya ushindi, hawataki kabisa kuzungumzia mapanga na mashoka
yaliyotembezwa jana na Green Guards!
Huwezi
kuzungumzia kushindwa au kushinda kwenye matokeo ya jana au mengine yoyote
yale, bila kujadili masuala hayo kwa upana sana, unless kama tumekubaliana kuwa
iwe ni sehemu ya demokrasia yetu, watu kukatwa mapanga, mashoka, damu
kumwagika, watu kukamatwa vituoni bila makosa, kisha CCM wakaachwa wanafanya
wanavyotaka, wakuu wa wilaya kuingia vituoni na kutoa maagizo.
Labda kwao
ni sehemu ya mchakato wa kuchagua wawakilishi! Vinginevyo basi tuanze kuwaandaa
Watanzania kwa uchafu wa namna hii.
Kwa kusema
haya kamwe haimaanishi kuwa CHADEMA haihitaji kufanya tathmini ya kitaalamu,
kitaaluma na kina sana. Itafanyika na itakuwa muhimu kwa ajili ya kuendelea
kujiimarisha na kujipanga katika mapambano haya.
Lakini kwa
vyovyote ni muhimu sana sana, kuweka mikakati ya kukabiliana na Intarahamwe
inayotaka kupandikizwa Tanzania na Watawala dhidi ya Watanzania.
Suala hili
la Green Guards kufanya maovu dhidi ya wapinzani wa CCM kwenye uchaguzi, tena
mahali pengine uovu wa kutisha unaohusisha silaha, kwa namna ile ile ya Intarahamwe,
mbele ya askari polisi, wala wasiguswe, wapo wengine bado wanaliona kuwa ni
jambo dogo au mzaha fulani hivi.
Siku madhara
yake yatakapokuwa yameshafika mfupani, tutajua Intarahamwe ilikuwa ni kitu
gani, kilianzaje, kilipataje nguvu na matokeo yake yalikuwa ni nini.
Where are
the voters, where is legitimacy?
Tumaini
Makene
Afisa
Habari-Chadema
No comments:
Post a Comment