Baadhi ya raia waliouawa ni pamoja na
David Yomami, Samuel Matiko, Robert Machumbe, Zakaria Marwa , Juma
Nyaitara, Juma Mwita, Marwa Mwita na Erick Makanya.
|
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda
Kamugisha, Kichune baada ya kukamatwa alikiri Polisi kuhusika katika mauaji ya
watu mbalimbali katika kata za Binagi, Turwa na Kitare katika vijiji vya
Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende na Rebu.
Kamanda Kamugisha alisema mtuhumiwa huyo Kichune alikamatwa Februari 6
mwaka huu mkoani Tanga baada ya Polisi
kufuatilia mtandao wake baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Baada ya kukamatwa, uchunguzi wa
Polisi ulibaini kuwa baada ya mauaji ya
watu tisa, mtuhumiwa alikodisha pikipiki kutoka kijiji cha Kenyamanyori
alikokuwa akiishi, hadi Musoma.
Alipofika Musoma, inadaiwa
alihifadhi bunduki aina ya SMG na risasi kadhaa kwa mshirika wake, Marwa Keryoba maeneo ya Bweri na
alipokamatwa alimtaja Keryoba kuwa ndiye
anayetunza silaha hiyo.
Februari 7 mwaka huu, Polisi
walifuatilia silaha hiyo kwa Marwa na kumkuta mtuhumiwa, ambapo alitakiwa
kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza
kurushia risasi askari.
"Marwa aliuawa Februari 7
alfajiri Bweri Musoma, wakati alipotakiwa kujisalimisha na kukaidi na kuanza
kurushiana risasi na askari," alisema Kamanda Kamugisha.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha,
kuna mtuhumiwa mwingine sugu wa mauaji ya watu zaidi ya 10, Senso Magabe
ameuawa katika majibishano na Polisi wiki iliyopita.
Hata hivyo katika majibishano hayo,
wenzake watatu walifanikiwa kutoroka na msako unaendelea wilayani hapa ambapo
wananchi wameombwa kutoa ushirikiano Polisi ili
kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kamanda Kamugisha alisema tayari
watu wanne waliokuwa katika mtandao huo wa ujambazi wamefikishwa mahakamani kwa
mashitaka ya unyang'anyi na mauaji.
Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani
ni pamoja na Kyoma Manguh, Marwa Mwita , Yohana Mgosi na Chacha
Bugichere ambapo kesi zao zitatajwa
Februari 19 mwaka huu.
Jana mamia ya wananchi wilayani
Tarime walifurika kuona mwili wa Kichune maarufu Kenonke ambaye amekuwa tishio
kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya Sh
milioni moja kwa
atakayetoa taarifa zitakazofanikisha
kukamata silaha za moto katika wilaya za Tarime na Rorya.
No comments:
Post a Comment