Na:-Nick Kilunga..:-Ni wanafiki tu ndo jina wanalopaswa kuitwa viongozi wetu wa Afrika,kwa miaka mingi wamekubali kuwa bendela fuata upepo wa siasa na ajenda za nchi za nchi za ulaya,Asia na mataifa makubwa (mabeberu)wa Magharibi ,ajenda ambazo huwa zinapenyezwa kwa siri na ustadi........... |
Na:-Nick Kilunga..:-Ni wanafiki tu ndo jina
wanalopaswa kuitwa viongozi wetu wa Afrika,kwa miaka mingi wamekubali kuwa
bendela fuata upepo wa siasa na ajenda za nchi za nchi za ulaya,Asia na mataifa
makubwa (mabeberu)wa Magharibi ,ajenda ambazo huwa zinapenyezwa kwa siri na
ustadi mkubwa na vyombo vyao vya kijasusi katika mataifa ya Afrika,kwa
kuwanunua viongozi wa kiafrika ambao siku zote bei zao zimekuwa kama
vocha,wengine hufikia mahala wakanunuliwa kwa wanawake na vipande vya Suti
tu,kwisha habari yao,wanapofushwa macho na ahadi zao zilizojaa ghiriba nyingi na
ulaghai,kiasi huondoa uwezo wao wa kufikiri sawasawa,kufikiri kma Waafrika,na
badala yake hutaka kufikiri na kuishi kma wazungu ama watu wa Asia,waafrika
lazima turudi kwenye mstari waliouchora kina Nyerere,Nkurumah,Senkolo,Ghandi,Luther King na kina wanaharakati kina Du
Bois,Afrika 4 Afrika and not others,tuirudishe Afrika mikononi mwetu waafrika
wenyewe(tafsiri yangu)tusiwaachie wazungu ambao daima hawana nia njema na mtu
mwafrika kma alivyowahi kusema rais wa Zimbambwe na mzalendo pekee wa Afrika
aliebaki,Mugabe kwamba kamwe tusimwamini mzungu hata mara moja labda uiamini
maiti yake akiwa amekufa,
Kwa mda mrefu mataifa ya ulaya,Asia na Magharibi
yamekuwa sio tu yakituamulia marafiki,mambo yetu bali wameenda mbali mpaka
kutuchagulia viongozi wamtakao,tujikumbushe vuguvugu la mapinduzi na mabadiliko
katika nchi za kiarabu,Tunisia,Misri,Libya,Siria nk,huko kote baada ya tawala
kubadilika tumeona rangi halisi za waliofanya mapinduzi hayo,japo siuungi mkono
pia ukatili na ubabe wa serikali nyingi kma iliyokuwa ya Ghadafi,Museven na
Kagame lakini siungi mkono siasa za mataifa makubwa kuingilia siasa za
Afrika,angalia jinsi watu wasivyo na hatia wanavyouawa huko Syria,Misri na sasa
AFRIKA YA KATI,CENTRAL AFRICA REPUBLIC,mauaji makali na ya kikatili kabisa
yanayondelea ,mauaji kati ya Waislamu waliowachache nchini humo dhidi ya
wakristo walio wengi,kwakweli ndugu zetu Waislamu wanauawa,wananyanyaswa na
kuumizwa kwenye nchi yao wenyewe nchi ya Asiri,nchi yao zamani waliokuwa
wakiishi kwa amani na ushirikiano mkubwa kati ya Waislamu na Wakristo kma
ndugu,leo wanauana kwa KWELI SIUNGI MKONO kinachoendelea huko wala Siwaungi
mkono wakristo wa Afrika ya kati,japo napinga misimamo ya dini kali kama
vikundi vya kidini kma Boko Haram lakini tuseme tu inatosha na waafrika tuamke
na kukomesha mauaji,
UNAFIKI WA SERIKALI NA TAWARA NYINGI ZA KIAFRIKA.
Imekuwa kawaida kwa nchi nyingi za kiafrika kuacha mgogoro ukue bila kuingilia kati kuutatua na mwisho wa siku mataifa ya magharibi yakiingilia kati iwe kijeshi ama kidiplomasia waafrika wamekuwa wakwanza wakipiga kelele kwamba wanaingiliwa mambo yao ya ndani kwenye serikali zao,nitakupa ushahidi,kwenye vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya mauaji mengi yalitokea nchi zilizokemea moja kwa moja zilikuwa chache tena na zenyewe zikiwa hadhina dhamira ya ndani na ya ukweli,tuliambiwa takribani watu 1500 waliuawa,juzi juzi mahakama ya kimataifa inayopambana na makosa ya Kivita na uharifu mkubwa walipoanza kamatakamata ya viongozi kazaa nchini Kenya na kuwapeleka mahakamani tunaona madiktekta wa kiafrika wakipiga kelele huo ni unafiki na uwoga,wakihofia na wao kutupwa huko sasa wameungana kichawi kuwapiga vta waendesha mashtaka wa ICC,lakini kwenye migogoro walikuwa kimya!

Tukashuhudia nchini Libya wakati rais wa nchi hiyo
akirusha madege yake ya kivita kuuwa raia,pindi akitumia vifaru na wadunguaji
wake mahiri kuzidungua roho za raia zake walikaa kimya,bt pale tu mataifa ya
nchi za magharibi zilipoazimia kuingilia kati na kuazimia kumwondoa madarakani
Ghadafi na hatimaye kuuawa wanafiki hawa wanaojiita marais na viongozi wa
Afrika wakaanza tena kupiga kelele zao za kinafiki kwamba mataifa ya magharibi
hayakupaswa kuchukua hatua hiyo ya kuingilia mambo ya ndani ya Libya na sasa
tunashudia kinachoendelea Libya ,Sudani zote kaskazini na kusini na Afrika ya
kati ,hasa kwa sasa tunashuhudia mauaji ya kutisha nchini humo bt hatuoni hatua
kali zinachukuliwa kama za kutuma vikosi vya kijeshi vya nchi za kiafrika
kuingilia kati na kuchora mstari wa Amani ambao utakuwa kimbilio la wanaokimbia
Vita hiyo,matokeo yake tunashuhudia majeshi ya Ufaransa ambayo nayo kimsingi
kuna madai yameshindwa kuwa fair na yamekuwa na upande na sasa umoja wa ulaya
unajianda kuingilia kati kwa kupeleka vikosi vyake huko ,huku mataifa ya
Kiafrika yakiwa kimya na viongozi wao wakiwa watazamaji wa kinachoendelea hii
ni AIBU SANA KWA WAAFRIKA NA VIONGOZI WAKE...Kwa leo naomba niishie hapa lakini
nitaendelea kuwasema hawa wanafika
wanaotutawala.
No comments:
Post a Comment