Simba SC yashindwa kuvunja rekodi uwanja wa nyumbani wa Mbeya City nakutoka sare ya 1-1 na Yanga SC yaibamiza 12-2 Komorozine. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 15, 2014

Simba SC yashindwa kuvunja rekodi uwanja wa nyumbani wa Mbeya City nakutoka sare ya 1-1 na Yanga SC yaibamiza 12-2 Komorozine.

Timu ya Mbeya City, leo Februari 15,2014, imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine kwa kulazimishwa sare kwa kufungana bao 1-1 na Simba SC, mchezo uliokuwa na kila aina ya upinzani uliomalizika huko Jijini Mbeya.
Bao la Simba SC lilifungwa na Amis Tambwe katika kipindi cha pili huku bao la Mbeya City, likipatikana kipindi cha kwanza katika Dakika ya 14 kwa mkwaju wa Penati ya Deogratius Julius.

Simba SC na Mbeya City sasa zimecheza Mechi mbili zaidi ya Vinara Azam FC, wenye Pointi 36, na Timu ya Pili Yanga, wenye Pointi 35, lakini wamebaki nyuma yao kwa Mbeya City kubaki Nafasi ya Tatu wakiwa Pointi sawa na Yanga lakini wana ubora wa Magoli hafifu huku Simba ikishika Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Mbeya City.

RATIBA/MATOKEO VPL 2013/2014.
Jumamosi Februari 15,2014.

Rhino Rangers 1 Mgambo JKT 1
Ashanti United 0 Kagera Sugar 0
Mtibwa Sugar 0 Tanzania Prisons 1
JKT Oljoro 0 JKT Ruvu 0
Mbeya City 1 Simba 1
Ruvu Shooting 1 Coastal Union 0

RATIBA MECHI ZIJAZO VPL 2013/2014.
Jumatano Februari 19,2014.

Tanzania Prisons v JKT Ruvu

Jumamosi Februari 22,2014.

Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons

Jumapili Februari 23,2014.

Simba v JKT Ruvu

HUKO KOMOROZINE:- Kwenye Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya Michuano ya CAF ya CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Leo Februari 15,2014, huko Uwanja wa Sheikh Said Mohamed International, Mitsamihuli, Visiwa vya Comoro, Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, wameitandika Komorozine de Domoni Bao 5-2 na kutinga Raundi ya Kwanza kwa Jumla ya Bao 12-2.

Wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Komorozine de Domoni Bao 7-0.

Katika Mechi ya Leo, Bao za Yanga zilifungwa na Hamis Kiiza, Dakika ya 13, Simon Msuva, Dakika ya 37, na Bao 3 za Mrisho Ngassa, kwenye Dakika za 22, 87 na 90.

Yanga SC sasa imesonga Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI ambapo watakutana na Mabingwa Watetezi, Al Ahly ya Misri, kati ya Februari 28 na Machi 2 na Marudiano kuchezwa kati ya Machi 7 na 9.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad