JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
Kufuatia
wito wa Serikali kuwa Wajumbe wote wanaombwa kufika Mjini Dodoma kuanzia tarehe
16 Februari, 2014 katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi,
Zanzibar wanapenda kuwaarifu Wajumbe wote maandalizi yafuatayo: -
1.0
USAFIRI
WA KUFIKA DODOMA
Wajumbe
wote wanatakiwa kujigharamia wenyewe kufika Dodoma kwa vyombo vya usafiri wa
umma. Wajumbe watarejeshewa gharama za
usafiri wa kufika Dodoma kutoka maeneo wanayotoka baada ya kuwasilisha
stakabadhi za gharama walizotumia kwa usafiri.
2.0
MALAZI
Utaratibu
wa malazi umeandaliwa. Hoteli
zilizoteuliwa kwa malazi kwa Wajumbe kuchagua kwa kadri itakavyowapendeza
zimeainishwa. Hoteli hizo ni hizi
zifuatazo: -
NA.
|
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
|
IDADI YA VYUMBA
|
MAWASILIANO
|
|
1.
|
Dodoma
Hotel - Mjini
|
87
|
0262321641
0262353782
|
|
2.
|
St
Gaspar Conference Centre - Kisasa
|
73
|
026235226
0767999903
|
|
3.
|
Hotel
Fifty Six - Viwandani
|
53
|
0757202630
0713702066
|
|
4.
|
Four
Points Hotel - Kisasa
|
20
|
026
2350214
0757 613270
|
|
5.
|
Peter
Palm Hotel
|
22
|
0767888311
0784888311
|
|
6.
|
Cana
Lodge - Mjini Barabara ya 9
|
17
|
026
2321199
0713
786611
|
|
7.
|
Dodoma
Grand Hotel - Majengo
|
20
|
026
2321187
|
NA.
|
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
|
IDADI YA VYUMBA
|
MAWASILIANO
|
8.
|
Kingstone
Lodge
|
17
|
026
2323057
|
9.
|
Hotel
DM - Majengo
|
19
|
0712
447325
|
10.
|
Golden
Glory Guest House - Area C
|
11
|
026
2353343
|
11.
|
Modern
Hotel - Area C
|
35
|
026
2304466
|
12.
|
Nam
Hotel - Area C
|
28
|
0756 652659
026
2354467
|
13.
|
Marryland
Hotel - Area C
|
20
|
0757
919166
|
19.
|
Giftland
Hotel - Area C
|
48
|
0762
159099
|
20.
|
Golden
Crown Hotel - Area C
|
27
|
0757
760333
|
21.
|
Joanic
Hotel - Kisasa
|
33
|
0653 867026
|
22.
|
Kidia
Vision Hotel - Mji Mpya
|
47
|
0262320095
0784520192
|
23.
|
VETA
Hotel
|
12
|
0756 698408
|
24.
|
Area
D Lodge - Area D
|
8
|
0764 698408
|
25.
|
Formula
One - Makole
|
8
|
0755 404621
|
26.
|
Summit
Hotel - Ipagala
|
42
|
0715 816000
|
27.
|
Kitemba
Hotel - Oneway
|
24
|
026 2323578
|
Wajumbe
watalipwa posho ya kujikimu na watalazimika kujitegemea kwa gharama za malazi
katika hoteli watakazofikia.
1.0
USAJILI
Zoezi
la Usajili litafanyika kwenye Ofisi ya
Bunge Mjini Dodoma kuanzia Saa Tatu Asubuhi tarehe 16 Februari, 2014 hadi
tarehe 17 Februari, 2014.
Zoezi
hilo litajumuisha Ujazaji wa Fomu ya Usajili, Upigwaji Picha za Vitambulisho na
Kukabidhiwa Begi lenye maelezo muhimu na stahiki nyinginezo kama
zitakavyoainishwa.
Wajumbe
wote wanapaswa kufika na nakala halisi ya vitambulisho vyao ili waweze
kutambuliwa kwa usajili.
Vitambulisho
vitakavyokubalika ni: -
(i) Shahada
ya Kupigia Kura;
(ii) Kitambulisho
cha Taifa;
(iii) Kitambulisho
cha Zanzibar;
(iv) Hati
ya Kusafiria;
(v) Leseni
ya Kuendeshea gari;
(vi) Kitambulisho
cha Mwajiri anayetambulika.
Iwapo
Mjumbe hana kitambulisho chochote kilichoainishwa hapo juu basi anaombwa
kuwasiliana na Maofisa waliotajwa katika Tangazo hili ili kuona namna anavyoweza
kusaidiwa.
1.0
MKUTANO
WA MAELEKEZO YA AWALI
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi
wameandaa Mkutano wa Maelekezo ya awali siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari,
2014 kuanzia Saa Kumi Jioni.
Wajumbe
wote wanapaswa kuhudhuria Mkutano huo bila kukosa ambao utajumuisha utaratibu
wa ukaaji, jiografia ya viwanja vya Bunge na huduma za utawala.
1.0
SHUGHULI
ZA KIKAO CHA KWANZA
Kikao
cha Kwanza kitafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 18 Februari, 2014 ambacho
kitajumuisha Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda atakayesimamia upitishwaji wa
Kanuni na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
2.0
MAWASILIANO
Kwa taarifa zaidi, Wajumbe wanaombwa kuwasiliana na:
Ofisi ya Bunge Maalum,
S. L. P. 901,
DODOMA.
Simu: 026 23 22
696
Fax: 026 23 23
116
Aidha, Wajumbe wanaweza kupata ufafanuzi zaidi kutoka
kwa Maafisa wafuatao:-
1.
Ndg.
John Joel
(0754
260 831)
2.
Ndg.
Amour Amour
(0777
855 878)
3.
Ndg.
Kitolina Kippa
(0754
363 237)
4.
Ndg.
Saidi Yakubu
(0762
089 225)
5.
Ndg.
Abdu Haji
(0779
894 847)
6.
Ndg.
Mossy Lukuvi
(0767 401 333)
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA KATIBU WA BUNGE NA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI
15
FEBRUARI, 2014
No comments:
Post a Comment