Mtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake
kwenye pikipiki kwa mpira.
|
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa
shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha
baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza
kumburuza mtaani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya
sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti
huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo
ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni
mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo
mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele
na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi
mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya
Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya
Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo
liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la
polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo
na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.
Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri
kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi
hadi sasa kwa upelelezi zaidi.
Na Valence Robert-Geita
No comments:
Post a Comment