Cheki Matokeo yote ya mechi za kwanza 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya,Chelsea FC akitoa sare na Real Madrid CF akishinda 6. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 27, 2014

Cheki Matokeo yote ya mechi za kwanza 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya,Chelsea FC akitoa sare na Real Madrid CF akishinda 6.


Mshambuliaji wa Galatasaray, Didier Drogba kushoto akipambana na Nahodha wa Chelsea, John Terry katika mchezo wa kwanza 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Februari 26,2014,usiku,kwa Chelsea ‘waling’ara’ baada kutoka Sare 1-1 huko Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi, Jijini Istanbul, Uturuki, walipocheza na Galatasaray Spor Kulübü.
Matokeo hayo ni nafuu kwa Chelsea hasa baada ya Klabu zote za Uingereza zinazoshiriki UEFA msimu huu, Arsenal, Manchester City na Manchester United, zote kupigwa Bao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 9 la Fernando Torres huku Katika Dakika ya 54, Galatasaray walisawazisha baada ya Kona ya Wesley Sneijder kukoswa na Jerry Terry na Aurelien Chedjou kuunganisha wavuni.


C.Ronaldo kulia na Bale kushoto wakishangilia moja ya mabao yao jana februari 26,2014 usiku wakati Real Madrid ikishinda goli 6-1 dhidi ya Schalke 04 na kutanguliza mguu mmoja hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi huo.

Wakicheza Ugenini huko Veltins Arena Jijini Gelsenkirchen Nchini Ujerumani, Real Madrid walishinda Mechi hiyo ya Kwanza ya UEFA kwa kuichapa Schalke Bao 6-1 kwa bao za Gareth Bale,Cristiano Ronaldo , Benzema kwa  kila mmoja kufunga mawili.

Schalke walifunga Bao lao pekee katika Dakika ya 90 Mfungaji akiwa Klaas-Jan Huntelaar.



Nao Manchester United  wakicheza huko Karaiskakis Stadium, Jijini Athens, Ugiriki na Olympiakos kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA walinyukwa Bao 2-0….kwa Bao za Olympiacos kufungwa na Alejandro Dominguez katika Dakika ya 38 na Joel Campbell, ambae ni Mchezaji wa Arsenal alieko Olympiacos kwa Mkopo, aliefunga kwa Shuti safi katika Dakika 55.

Man United ni Timu ya 3 ya Uingereza katika UEFA, kufuatia Man City na Arsenal, kuchapwa 2-0 kwenye Raundi hii lakini tofauti yao ni kuwa wao wamefungwa Ugenini na watarudiana Nyumbani hapo Machi 19,2014, Man City na Arsenal zitasaka ushindi wa Ugenini kwenye Mechi za Marudiano.


UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Bora.

MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 11,2014.

22:45 Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]

Jumatano Machi 12 ,2014.

22:45 FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]

Jumanne Machi 18,2014. 

22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]

Jumatano Machi 19 ,2014.

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad