Cheki mafunzo ya ukocha ,uamuzi na uongozi katika mchezo wa mpira wa wavu mkoani Kagera yakifanyika wilayani Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 18, 2014

Cheki mafunzo ya ukocha ,uamuzi na uongozi katika mchezo wa mpira wa wavu mkoani Kagera yakifanyika wilayani Ngara.


Washiriki 37 kutoka wilaya 7 za mkoa wa Kagera isipokuwa Biharamulo wa Mafunzo ya ukocha ,uamuzi na uongozi katika mchezo wa mpira wa wavu mkoani Kagera wakimsikiliza kwa Makini mkufunzi wao Mwl.Somo Ahmed Kimwaga kutoka kamati ya ufundi ya mchezo wa Wavu ya TAVA Taifa,katika mafunzo ya siku 7 yanayofanyika katika ukumbi wa mkuu wa wilaya ya Ngara.

Kutoka kulia ni  Afisa elimu shule za sekondari wilaya ya Ngara aliewakilishwa na Jona Katanga,Afisa elimu shule za Msingi Saimoni Mumbee,mgeni rasmi Katibu tawala wilaya ya Ngara Tibaijuka na Afisa Michezo na Utamaduni wilaya Salumu Bakari wakifatilia mafunzo hayo kwa wadau wa mchezo wa Wavu mkoani Kagera.
Mwl.Somo Ahmed Kimwaga kutoka kamati ya ufundi ya mchezo wa Wavu ya TAVA Taifa,akitoa elimu juu ya sheria mbalimbali zinazotawala mchezo wa wavu.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Katibu tawala wa wilaya ya Ngara Vedastus Josephat Tibaijuka na kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia elimu wanayoipata kuimalisha mchezo wa wavu sambamba na kuinua vipaji vya mchezo huo katika maeneo yao.

Makamu mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Wavu mkoani Kagera KAREVA Dauson Buninange amesema mafunzo hayo yanashirikisha  washiriki  37 kutoka wilaya 7 ,ukiondoa wilaya ya Biharamulo ambayo haikutuma wawakilishi na kuwaomba wadau wa michezo mkoani Kagera kutoegemea mchezo mmoja tu wa soka na badala yake pia wautazame na mchezo wa Wavu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad