Hali ya
taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji la Arusha
kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina
asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo.
Mamia ya
wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi
walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza
na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin
Mbise alisema:-“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona
kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa
akiwa uchi wa mnyama.
Wananchi
wakishuhudia tukio hilo huku
baadhi yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
|
“Wengi
tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo
alitoweka, badala yake mle mwenye ungo
mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana.
Mbise
alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua
kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai. Wananchi
wakishuhudia tukio hilo.
Hata hivyo,
alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na
petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi yao
wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya
wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa
Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi
huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia
tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo
walithibitisha.
Habari kwa hisani ya :-Global Publisher.
No comments:
Post a Comment