Yakiwa
yamebaki masaa machache kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza mjini hapa,
Chama cha Mapinduzi kimesema kitaendelea kusisitiza mfumo wa serikali mbili
kufuatia kikao cha siku mbili cha Halmashauri yake Kuu ya Taifa (NEC).
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokutana na
wanahabari kuzungumzia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika mfumo wa
sasa wa kiserikali.
“Changamoto
zote tumezitafakari [tukaona] jibu lake sio serikali tatu,” alisisitiza Bw.
Nnauye akiongeza “Bado sisi ni waumini wa serikali mbili.”
Hata
hivyo, msemaji huyo wa CCM alikiri kuwa ili mfumo huu wa serikali mbili
uendelee kufanya kazi, lazima baadhi ya mambo yabadilike. “Sio serikali mbili
kama zilivyo sasa,” alisema.
Bw. Nnauye
anaamini NEC imejiandaa vyema kuwasilisha hoja nzito zinazojibu maswali magumu
kuhusu mapungufu ya utaratibu wa sasa wa serikali mbili.
Hata
hivyo, hakuwa tayari kuzitaja hoja hizo, akisema zitawekwa wazi wakati wa Bunge
la Katiba.
Kusikiliza
kauli rasmi tazama VIDEO juu.
No comments:
Post a Comment