Kipa wa
akiba Lukasz Fabianksi aliingia badala ya Cazorla akaenda kusimama langoni, na
tangu hapo Arsenal wakalazimika kucheza mchezo wa kujihami.
|
Wachezaji wa
Bayern wakimpongeza Kroos baada ya kufunga bao la kwanza Emirates, baada ya
kuilaza Arsenal mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
|
Timu ya Bayern
Munich imeendeleza ubabe wake, baada ya kuilaza Arsenal mabao 2-0 kwenye Uwanja
wa Emirates mjini London jana Februari 19,2014,usiku katika mchezo wa kwanza
hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bao hilo pekee lililoizamisha Arsenal iliyomaliza pungufu ya mchezaji mmoja, lilipatikana dakika ya 54, mfungaji Toni Kroos aliyefumua shuti kali akiwa umbali wa mita 20 baada ya pasi ya Philipp Lahm.
Dakika ya 8
Mesut Ozil aliangushwa na Boateng na Penati kutolewa lakini Penati hiyo
iliyopigwa hafifu na Ozil iliokolewa na Kipa Manuel Neuer ambae ni Rafiki wa
Ozil tangu utotoni.
Kwa Ozil
hiyo ni Penati yake ya Tatu mfululizo kukosa akichezea Klabu, nyingine zikiwa
Arsenal ilipocheza na Marseille kwenye Makundi ya UCL Msimu huu na kabla wakati
akiwa na Real Madrid.
Kwa kawaida
Wapiga Penati wa Arsenal ni Olivier Giroud na Mikel Arteta na wote hawakuwamo
kwenye Mechi hii.
Kwenye
Dakika ya 37 Toni Kroos alipenyeza pasi ya juu kwa Arjen Robben ambae
alichomoka na kuipita Difensi na kukontroli Mpira akimhadaa Kipa Wojciech
Szczesny ambae alimwangusha na Refa Nicola Rizzoli toka Italia kutoa Penati na
Kadi Nyekundu kwa Szczesny.
Lakini David
Alaba alikosa Penati hiyo iliyopiga Posti chini na kutoka huku Kipa wa Akiba,
Fabianski, alieingizwa baada kutolewa Santi Cazorla ili kukaa langoni ‘akienda
mbovu’.
Katika
Dakika ya 54, baada kupokea pasi safi toka kwa Nahodha Philip Lahm, Toni Kroos
aliachia shuti toka Mita 20 ambalo lilipita juu kulia na kutinga wavuni na
kuwapa Byern Munich Bao safi.
Kwa ushindi
huu wa Bao 2-0, Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich wamejiweka katika hali njema
kucheza Robo Fainali na Arsenal wanahitaji kushinda 3-0 huko Munich ili
wapindue kipigo.
Timu hizi
zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich, Germany hapo Machi 11,2014.
Nao AC Milan
wakicheza dhidi ya Atletico Madrid walijikuta wakinyukwa kwa bao la dakika ya
82 kwa kichwa cha Straika hatari Diego Costa na kuwapa Atletico Madrid ushindi
wa Bao 1-0walipocheza Ugenini huko San Siro na AC Milan katika Mechi ya Kwanza
ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA Ligi.
Raundi ya
Mtoano ya Timu 16:-RATIBA.
[Saa za
Bongo]
Jumanne
Februari 25,2014.
20:00 Zenit
St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45
Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano
Februari 26 ,2014.
22:45
Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45
Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
No comments:
Post a Comment