|
Rais JK
akielekea kukagua daraja la Dumila lililokatika kutokana na mvua kubwa
iliyonyesha eneo hilo Januari 22, mwaka huu wilayani Mvomero, Morogoro.
|
Rais
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na
Usalama,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa
Tanzania
(JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu
walioathiriwa
na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia
ujenzi wa
nyumba za muda wa wahanga hao.
Rais
pia
ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako
wahanga hao
wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.
Aidha,
Rais Kikwete
amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali
itahakikisha
inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula,
malazi, maji
na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza
kujitegemea
tena.
Rais
Kikwete
ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea
kambi za
wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi
yaliyoko
Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji
cha Mateteni
kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.
Katika
hotuba zake
fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao
wanalala,
Rais Kikwete amesema ameagiza
Jeshi
kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa
taratibu za
kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.
“Kazi
yetu ni
kusimamia maisha ya watu hasa
kipindi cha
shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za
Kiserikali
za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika.
Ndiyo
maana
nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka
makazi ya
muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika
mazungumzo
hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia
maji ili
kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya
sasa maji
yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”
Kuhusu
upatikanaji
wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa
Serikali
inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha
na hata kile
tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili
tupate fedha
za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu
malazi, Rais
amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa
yanapatikana
na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini
na waje
kupata vichomi.”
Kuhusu
maji, Rais
Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure
kwa wahanga.
“Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya
maji
itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu
huduma za
afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo
huduma ya
afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi
kwenye
makambi.
Rais
ameagiza
kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika
wakae chini
ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta
mwafaka
kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza
kupatiwa
maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.
“Hili
ni lazima
kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa
kutokea ni
dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu
kwa sababu
zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya
kurudi ama
kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”


.jpg)



.jpg)
.jpg)



No comments:
Post a Comment