Mchezaji
huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya
Uingereza, na ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika
orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang,
Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.
Orodha fupi
ya waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote
barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano
na wenzake katika timu, na kwa kucheza mchezo safi na kwa haki.
Kisha,
kupitia idadi kubwa kabisa kuandikishwa kwa wapiga kura, mashabiki waliweza
kushiriki katika shughuli hiyo katika mtandao, au kupitia ujumbe wa simu ya
mkononi.
Mashabiki
hao wameamua kwamba Toure ndiye bora zaidi, kwani katika kipindi cha mwaka
mmoja uliopita, raia huyo wa Ivory Coast alicheza kwa bidii, kuonyesha mchezo
wa kasi, ubunifu, na vile vile kwa kufunga magoli.
Ingawa mwaka
2013 ulikuwa ni wa ufanisi kwa Toure hasa kwa kupata vikombe, hakuweza
kuisaidia nchi yake, wala klabu, kupata kombe lolote lile, lakini bado alionyesha
kiwango cha hali ya juu katika mchezo.
Baada ya
kuvunjika moyo kwa kushindwa kuutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Premier wa
mwaka 2012 akiichezea Manchester City, Toure alirudi uwanjani akijizatiti, na
kuimarisha mikwaju yake ya free-kick.
Alitumbukiza
wavuni bao, kwa mpira wa kupinda, katika siku ya kwanza ya msimu mpya wa ligi
kuu ya Premier, wakati timu yake ilipocheza na Newcastle, na akarudia hayo hayo
katika mechi iliyofuata wakati Hull walipowatembelea katika uwanja wao wa
nyumbani.
Toure amefunga
magoli manne ya kupanga kwa makini shambulio, na hayo yakiwa ni kati ya magoli
saba kwa jumla aliyoweza kuifungia klabu ya Man City msimu huu.
Kufikia
sasa, mwaka huu wa 2013, Toure ametumbukiza wavuni jumla ya magoli 12; ya klabu
na vile vile ya nchi yake, na hiyo ni rekodi nzuri sana kwa mchezaji wa kiungo
cha kati.
Mbali na
ustadi huo katika kumalizia, Toure ni kiongozi bora katika timu, na maarifa
yake yameiwezesha City kufikia sasa kuwa katika nafasi ya nne katika ligi kuu
ya England.
Aliisaidia
kikamilifu nchi yake ya Ivory Coast kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia ya
mwaka ujao itakayofanyika nchini Brazil.
Timu yake ya
Tembo, The Elephants ilihitaji kuusahau mwanzo mbovu hapo
awali katika kampeni yao ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na
walipoondolewa katika robo fainali na Nigeria, ambao hatimaye waliibuka
mabingwa, na Toure akiwapa matumaini ya kufanya vyema baadaye.
Nje ya
uwanja, Toure ameongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi katika soka, hasa baada
ya matusi kuelekezwa kwake katika mechi ya ligi ya klabu bingwa dhidi ya CSKA
Moscow, mwezi Oktoba, na akionyesha moyo wa uvumilivu na wa kimichezo
unaostahili uwanjani.
Tukio kama
hilo linaweza kumvunja moyo mchezaji asiyejiamini, lakini Toure ameendelea kuwa
mchezaji wa kipekee tangu wakati huo.
Na katika
mwaka wa tano baada ya jina lake kupangwa katika orodha ya wachezaji wanaowania
tuzo, hatimaye Toure ametajwa kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora zaidi wa
soka barani Afrika.
kwa hiyo Idhaa
ya Dunia ya BBC ilitangaza orodha ya wachezaji kutoka Afrika watakaowania tuzo
ya BBC ya mwanasoka bora wa mwaka 2013 ijulikanayo kama "BBC African
Footballer of the Year award".
Wachezaji
waliotajwa na wataalam wa masuala ya soka kuwania tuzo hiyo ni:-
1.Pierre-Emerick
Aubameyang - mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon na Borussia Dortmund ya
Ujerumani.
2.Victor
Moses - wa timu ya taifa ya Nigeria na Liverpool ya England akiwa katika mkopo
kutoka timu ya Chelsea pia ya England.
3.John Obi
Mikel - mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Chelsea ya England.
4.Jonathan
Pitroipa -mchezaji wa Burkina Faso na Rennes ya Ufaransa.
5.Yaya Touré
- mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na pia timu ya Manchester Cityya
England.
Kazi ya
kuwapigia kura wachezaji hao ilianza tarehe 11 Novemba 2013 saa nane na dakika
arobaini na tano kwa saa za Afrika Mashariki, wakitangazwa katika kipindi cha
asubuhi cha BBV cha Newsday.







No comments:
Post a Comment