Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro ateuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 04, 2013

Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro ateuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania.


Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi (CCM).


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
              press@ikulu.go.tz             
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr.Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.

Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.


3 Desemba, 2013.


Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.


Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.


Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo , mjini Mbalizi mkoani Mbeya,Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad