Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini yawatandika goli 9-0 wenzao wa Kumunazi wakiwa Nyumbani kwao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 19, 2013

Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini yawatandika goli 9-0 wenzao wa Kumunazi wakiwa Nyumbani kwao.

Kikosi cha Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wao wa kirafiki wa kujipima nguvu  dhidi ya wenzao wa Kumunazi.


Katika mchezo huo Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini liondoka na ushindi mnono wa bao 9-0 ,goli zikifungwa na Farida Zakaria ,Sara Jonston na Magreth Anton wakifunga magoli 2 kila mmoja ,Nsia Faustine,Agnes Scot na Cossy Amandus wakifunga goli moja moja katika mchezo huo.

Kikosi cha Timu ya Soka ya Wanawake ya Kumunazi kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wao wa kirafiki wa kujipima nguvu  dhidi ya wenzao wa Ngara Mjini.


Afisa Utamaduni na Michezo Salum Bakari akifungua mchezo huo alizitaka timu zote kucheza kwa amani bila fujo na kusema kuwa mchezo huo pia una lengo la kupata wachezaji watakaounda timu ya Wanawake ya wilaya itakayoenda ziara ya kimichezo wilayani Biharamulo hivi karibuni.
Kutoka kushoto ni Mratibu wa Soka la Wanawake wilaya ya Ngara na Diwani Viti Maalum (CCM) Ninia Bakari  na Saidi Salum(mwenye shati jeupe) ambaye ni Afisa Michezo wilaya ya Ngara  nao walipata fursa ya kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa Kumunazi kwa Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini kuwatandika magoli 9-0 wenzao wa Kumunazi.

Ni kocha wa Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini Mbaruku Hussein pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa Wadau wa michezo Mkoani Kagera kuijitokeza kuifadhiri timu hiyo vifaa vya michezo ili iweze kufanya vyema katika mashindano mbalimbali.





Muonekano wa mashabiki mbalimbali waliojitokeza kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa kumunazi,kata ya Kasulo licha ya mvua kubwa pia kunyesha  walifanikiwa kutazama timu yao ya kumunazi ikitandikwa mabao 9-0  kutoka kwa Timu ya Soka ya Wanawake ya Ngara mjini.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad