Hayo ni kwa
mujibu wa ripoti ya kila mwaka iliyotolewa Jana ( Desemba 03,2013) na Shirika
la Kimataifa la kupambana na Ufisadi la Transparency International.
Shirika hilo
limesema kuwa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya thuluthi mbili ya nchi
zinaghubikwa na ufisadi, ni hali ambayo itaathiri ukuaji wa uchumi na
kukwamisha vita dhidi ya umaskini na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu
wa Shirika la Transparency International – TI lenye makao yake mjini Berlin,
kuwa karibu asilimia 70 ya mataifa yote ulimwenguni yanafikiriwa kukabiliwa na
“tatizo kubwa” la ufisadi katika sekta ya umma, na hakuna moja kati ya nchi 177
zilizofanyiwa utafiti mwaka huu iliyopata alama nzuri.
Orodha ya
kila mwaka ya TI ndicho kipimo kinachotumiwa zaidi kuangazia ufisadi katika
vyama vya kisiasa, polisi, mifumo ya mahakama na utumishi wa umma, janga ambalo
lina athari juu ya hatima ya maendeleo ya nchi na vita dhidi ya umaskini.
Maskini ndio
wanaoumia.
“Ufisadi
unawaumiza sana watu maskini” amesema Mtafiti mkuu Finn Heinrich, na kuendelea
kueleza kuwa hicho ndicho unachokiona wakati unapoziangalia nchi zilizoshika
mkia kwenye orodha.
Ndani ya
nchi hizo, amesema mtafiti huyo, watu maskini ndio wanaoumia sana, na nchi hizo
kamwe haitaweza kuondoka katika janga la umaskini ikiwa hazitapambana na
ufisadi.
Miongoni mwa
nchi ambazo zimeshuka zaidi kwenye Ripoti ya Orodha ya Ufisadi mwaka wa 2013 ni
Syria inayokabiliwa na vita, pamoja na Libya na Mali, ambazo pia zimekabiliwa
na migogoro ya kijeshi katika miaka ya karibuni.
Miongoni mwa
nchi “zilizopiga hatua nzuri”, ijapokuwa kutoka kiwango cha chini, ni Myanmar,
ambako utawala wa kijeshi umefungua milango ya mchakato wa demokrasia na huku
ikineemeka na nafasi kubwa ya uwekezaji, na kugeukia zaidi sheria za uwazi na
uwajibikaji.
Heinrich
anasema hiyo ndiyo njia pekee nchi zinaweza kuepuka “laana ya raslimali” ambako
raslimali hupatikana tu kwa walio wachache na wenye uwezo.
Nigeria, na nchi
nyingine zenye utajiri wa mafuta bila shaka ni mifano mizuri.
Nchi zenye
migogoro zinaongoza kwa rushwa.
Nchi
zilizoorodheshwa katika nafasi za mwisho ni pamoja na Iraq, Syria, Libya, Sudan
na Sudan Kusini, Chad, Guinea ya Ikweta, Guinea Bissau, Haiti, na Yemen.
Nazo
nchi zilizofanya vyema ni Denmark, New Zealand, Luxembourg, Canada, Australia,
Uholanzi, Uswisi, Singapore, Norway, Sweden na Dinland.
Rwanda iliyo
katika nafasi ya 49 ulimwenguni imetajwa kufanya vyema katika eneo la Afrika
Mashariki ikifuatwa na Tanzania iliyo katika nafasi ya 111, Kenya katika nafasi
ya 136, Uganda inayokuja katika nafasi ya 140, na Burundi iliyo kwenye nafasi
ya 157.
Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo inajikuta katika nafasi ya 154 kwenye orodha hiyo.
Heinrich
amesema ufisadi unahusishwa na nchi zinazosambaratika kutokana na migogoro na
ambazo serikali haziendeshwi kikamilifu na hivyo watu ni lazima watumie kila
mbinu kuendesha harakati zao, kupata huduma, kupata chakula na kuishi.
Mtafiti huyo
amesema Afghanistan ambako majeshi mengi ya magharibi yanayoongozwa NATO
yanaondoka mwaka ujao baada ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya mwongo mmoja, ni
“hadithi ya kutisha”.
Kwa sababu
hawajaona mabadiliko yoyote makubwa. Nchi za magharibi zinawekeza kiasi kikubwa
siyo tu katika masuala ya usalama lakini pia zinajaribu kurejesha mkondo wa
sheria, lakini bado utafiti wa miaka ya karibuni unaonyesha kuwa idadi ya watu
wanaotoa hongo bado ni ya juu kabisa ulimwenguni.
Source:Dw.






No comments:
Post a Comment