 |
PUMZIKA KWA
AMANI BABU MANDELA:-ambapo Nchi ya Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo
kuanzia tarehe 06 hadi 08 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa
Afrika Kusini,
Mzee Nelson Mandela.
|
MANDELA:-Tangu
maisha yake ya upole hadi kuwa kiongozi wa dunia: Nelson Mandela alikuwa
wakili, mwanaharakati na mfungwa kabla ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini. Akiwa anasifika ndani ya nchi yake kama 'Madiba' ,Bwana Mandela
aliwatia moyo sana watu kote duniani.
 |
Mzee Mandela ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma
na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa
moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
|
 |
Miaka ya
Mapema ya 1952:-Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji
kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe
18 Julai mwaka 1918.
Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule.
Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson.
Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema.
Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin
Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC).
|
 |
Kesi ya
Uhaini mwaka 1956:-Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza
ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano
na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa
uwakilishi.
Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC
ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake
kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye
pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa
mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.
|
 |
Kufungwa
Maisha mwaka 1964:-Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua
waandamanaji 69 mjini Sharpville mwaka 1960.
Serikali ilihofia kuwa wangelipiza
kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha
harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.Mwaka 1962,
Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama wengine
wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na
wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964.
|
 |
Huru
hatimaye mwaka 1990:-Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya
ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka
1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, Rais FW De Klerk
akakiondolea marufuku chama cha ANC.
Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa
baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe
wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka
uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya
kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.
|
 |
Tuzo ya
amani ya Nobel 1993:-Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo,
walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini.
Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila tuwezalo kuweza
kuleta mageuzi duniani.''
|
 |
Rais mpya
mwaka 1994:-Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika
Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa
kidemokrasia. Mandela alichaguliwa.
Akihutubia umma, katika sherehe ya
kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale,
Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za
kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki
alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.
|
 |
Akitoka
Robbben mwaka 1995:-Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson
Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa
miaka 18.
Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa
wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya
Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya
mawe.
|
 |
'Usiniite''2004:-Thabo
Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na
hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa
aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80.
Aligunduliwa kuwa na saratani ya
Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu,
akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha
aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.
|
 |
Sherehe ya
siku ya kuzaliwa kwake mwaka 2008:-Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa
waliungana na Mandela katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London
kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika,
aliwaambia, ''ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu
sasa.''
|
 |
Kuugua mwaka
2010:-Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa
alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010
nchini humo.
Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku
serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea
matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .
|
Tanzania
imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013,
kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya
Kikwete pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu
bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia
kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa
Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote
na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela
kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 |
Rais wa
zamani wa Afrika Kusini,
Mzee Nelson
Mandela.
|
Rais
ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika
ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa
wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini
kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na
mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais
amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo
wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa
Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya
ubaguzi wa rangi.
"Mandela
ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni
wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake
wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi
wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu
ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela
amefariki huko Johannesburg nchini Afrika ya Kusini akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye
aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi
baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela
alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini
kwa miezi mitatu.
Katika
taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela
amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma
amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mzee Mandela
aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais
aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka
gerezani.
Chanzo:-
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment