Meli ndogo ya mizigo yazama Kilwa Masoko:- mmoja ahofiwa kupoteza Maisha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 14, 2013

Meli ndogo ya mizigo yazama Kilwa Masoko:- mmoja ahofiwa kupoteza Maisha.

Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo katika bandari ya Kilwa masoko.

Akiongea na Globu ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia (Desemba 08,2013)  ambapo Nahodha wa Meli hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana.

Taarifa zaidi => http://bit.ly/1jzyS4J

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad