Mama mmoja ajeruhiwa kwa kumwagiwa maji ya moto mwili mzima na jirani yake kisa Wivu wa Kimapenzi . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 14, 2013

Mama mmoja ajeruhiwa kwa kumwagiwa maji ya moto mwili mzima na jirani yake kisa Wivu wa Kimapenzi .

Bi Neema Teti, akiwa amelazwa katika wodi ya Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa maji ya moto na jirani yake aliyemtuhumu kuwa anatembea na mume wake jijini Arusha..Picha /Habari  Na Gadiola Emanuel –Arusha.
Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Jijini Arusha, Bi. Neema Teti, amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 

Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho aliyetambulika kwa jila na Mama Tatu Msuya, ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.

Majeruhi huyo amelazwa katika wodi ya wagonjwa majeruhi ya hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Akielezea tukio hilo, Neema alisema kuwa alikutwa na maswahibu hayo wiki iliyopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya.

Aidha alisema kuwa alitumwa mtu kumuita afike nyumbani kwa mtekelezaji kwa ajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kummwagia maji ya moto.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru, Neema Bayo, amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. 

Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru, Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yanazidi kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini, bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini.

Naye Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha, Maria Maswa, akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya Mount Meru, amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuwaji wa matatizo hayo.

Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea kumsaka Mama Tatu Msuya, anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho na kutokomea kusikojulikana.

pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad