Kampeni ya
kitaifa Nchini Tanzania ya kuwaondoa wahamiaji haramu iliyopewa jina la “Operesheni
Kimbunga” awamu ya pili ambayo inaendelea katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya
Ziwa, imewanasa majambazi watano wanaojishughulisha na biashara ya kuuza silaha
zinazotoka nchi jirani na kuziingiza nchini.
Naibu Kamishna wa operesheni hiyo, Simon Sirro, aliyasema hayo Octoba 02,2013, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bukoba, mkoani Kagera, kuhusu maendeleo ya operesheni hiyo.
Naibu Kamishna wa operesheni hiyo, Simon Sirro, aliyasema hayo Octoba 02,2013, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bukoba, mkoani Kagera, kuhusu maendeleo ya operesheni hiyo.
Alisema hadi sasa, majambazi 88 wamekamatwa miongoni mwao, watano wanaojihusisha na biashara ya kwenda nchini Burundi kununua silaha kwa shilingi 300.000 na kuziingiza nchini na kuziuza kuanzia shilingi Milioni moja.
Alisema operesheni hiyo awamu ya pili, ilianza Septemba 21 hadi Oktoba Mosi mwaka huu ikiwa na mafanikio makubwa ambapo wahalifu 529 walikamatwa na wahamiaji haramu 425 katika Mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera.
Aliongeza kuwa, walioruhusiwa kwa uamuzi wa mahakama ni 159, waliorudishwa makwao kwa hiari 122, walioachiwa huru 39 na wanaoendelea kuhojiwa hadi sasa 105.
Kamanda Sirro alisema, watu watano wanashikiliwa kwa tuhuma ya kuwatorosha na kuwahifadhi wahamiaji na majangili 11 ambapo silaha mbalimbali 23 zimekamatwa.Silaha hizo ni pamoja na bunduki aina ya SMG, bastola, magobole 18, magazine mbili, bomu la kutupwa kwa mkono pamoja na sare moja ya Jeshi la Burundi.
Operesheni
hiyo inayoendelea katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Ggeita chini ya Mkuu wa
operesheni za jeshi la polisi Tanzania, naibu Kamishna Simon Sirro, pia
imewanasa jumla ya wahamiaji haramu 425, wakiwemo raia wa Burundi 180,
Wanyarwanda 149, Waganda 82 na Wakongomani 14 , na kufanya jumla ya wahalifu wa
makosa mbalimbali waliokwisha kamatwa kufikia 529 wakiwemo wahusika wa mtandao
wa ujambazi wa kutumia silaha katika kipindi cha siku 10.
Kuhusu
ng'ombe 103 mali ya Bw. Kalemela George ambao wametaifishwa kwa amri ya
mahakama ya wilaya ya Biharamulo kwa kosa la kukutwa ndani ya hifadhi ya taifa
ya Burigi na wengine 220 waliokamatwa kwenye hifadhi ya Kimisi wilayani
Karagwe, naibu kamishna wapolisi Simon Sirro akatumia wasaa huo kuwaalika
wananchi wanaohangaika kutafuta ng'ombe wa kuchinja kuchangamkia soko kwenye
maeneo ya operesheni, kwani ng'ombe ni wa kumwaga.
Akizungumza
kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Fabian Masawe, wakati wa operesheni
Kimbunga, Mkuu wa wilaya ya Kyelwa ,Kanali mstaafu Issa Njuki amesema kwamba
vyombo vya ulinzi na usalama ngazi zote vimepewa jukumu la
kuwabainisha popote walipo wahamiaji haramu na kisha kukusanywa na kuwekwa
sehemu moja na baadaye kuhojiwa ili ambao watabainika si raia warejeshwe kwenye
nchi zao wanakotoka.





No comments:
Post a Comment