Abiria
hamsini na moja waliokuwa wakisafiri na basi la Taqwa kutoka Bujumbura Nchini Burundi na
kuelekea jijini Dar-es-Salaam Nchini Tanzania wametekwa katika kijiji cha Milade wilayani
Mkalama Mkoani Singida na kuporwa mali , simu na fedha zaidi ya shilingi milioni mia mbili
hamsini.
Akieleza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida Bw. Godfrey Kamwela amesema watekaji
hao waliwaamrisha abiria kushuka chini ya basi baada ya kuvunja vioo na kuanza
kuwasachi na kufanikiwa kupora simu, fedha za kitanzania shilingi milioni
tano ,dola za kimaerekani dola laki moja elfu sitini na faranga zenye
thamani ya elfu ishirini.
Kufuatia tukio hilo,Kamanda Kamwela amewaomba wananchi
na makampuni ya simu kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuweza kuwa kamata
watu ambao wamefanya tukio hilo.
Kwa upande
wake Dereva la basi hilo Bw. Ahamed Seif amesema gafla aliona majani
barabarani na alipoangalia vizuri aliona kuna mawe makubwa mawili
yakiwa barabarani na kushindwa kuyakwepa ,baada ya kugonga mawe hayo
magurudumu yote mawili ya mbele yalipasuka na gari ikaserereka umbali wa
mita mia moja.
Kwa upande
wao abiria na majeruhi wamesema waliona gari likipoteza mwelekeo na baadaye
walisikia sauti za watu zikiwaambia washuke na watoe fedha na simu zao,lakini
abiria wengine wamewatupia lawama wafanyakazi wa basi hilo kuchukuwa abiria
wa njiani wakati basi likiwa limejaa na abiria hao inasadikiwa ndio waliokuwa
wakiwasiliana mara kwa mara na watekaji.
Naye mganga wa
wodi ya majeruhi ya hospitali ya mkoa wa Singida Dkt Banuba Deogratias amesema
walipokea majeruhi kumi na tisa walikuwa na mipasuko na majeraa ya
kupigwa na fimbo, wameweza kuwatibu na kuruhusiwa isipo kuwa wengi wao hawana
fedha kwa sababu ni raia kutoka nchi za Burundi na Kongo walikuwa
wakisubiri kukabidhiwa kwa idara ya ustawi wa jamii ili wasaidiwe nauli
za kurudi makwao.






No comments:
Post a Comment