Mcheki Ray C na Ujio wake mpya ndani ya muziki wa Bongo Fleva Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 27, 2013

Mcheki Ray C na Ujio wake mpya ndani ya muziki wa Bongo Fleva Nchini.

Staa wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Rehema Chalamilla 'Ray C', akiingiza sauti ndani ya Studio za THT, chini ya maprodyuza Emma The Boy na Tudy Thomas,ambao wamepania kumrejesha katika game kwa kishindo msanii huyo, ambaye alipotea kwenye ulimwengu wa Burudani baada ya kutopea katika utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa sasa ameachana nayo na kumrudia mwenyezi Mungu sambamba na kuendelea kutumia dozi ya kuondoa sumu ya madawa hayo.

Ray C akiingiza sauti tayari kwa maandalizi ya ujio mpya kwenye game la Bongo Fleva.

Prodyuza  Tudy Thomas (kulia), akijadiliana jambo lililotokana na majadiliano ya kuboresha ngoma mpya ya Ray C, pichani kati ni  Emma The Boy akipiga mzigo tayari kwa kumkamilishia Ray C ngoma yake mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.

Ray C, akijaribu kutoa akapela kwa Maprodyuza hao, wakati wakiendelea kuiboresha ngoma yake mpya.

Ray C, akiwa katika pozi ndani ya studio hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad