![]() |
Mkurugenzi
Mkuu wa TMA Nchini,
Dk. Agness
Kijazi
|
MAMLAKA
ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetahadharisha kuwepo kwa kimbunga katikati ya
bahari kitakachosababisha mvua nyingi za muda mfupi.
Kwa
sababu hiyo mamlaka imewataka wakulima kwenye baadhi ya mikoa hasa ya kaskazini
mwa nchi na iliyopo ukanda wa Ziwa Victoria kupanda mazao yanayostahimili ukame
na kukomaa mapema.
Viashiria
vya vimbunga hivyo vinasababishwa na joto la bahari kupungua na hivyo
kusababisha mvua nyingi za muda mfupi kwa baadhi ya maeneo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana (Septemba 06,2013) , Mkurugenzi Mkuu wa
TMA, Dk. Agness Kijazi, aliwashauri wakulima wa mikoa ya kaskazini mwa Dodoma,
Singida na Tabora kutafuta ushauri wa maofisa ugani wa maeneo hayo kwa vile
inatabiriwa kuwa na unyevunyevu hafifu kwa kipindi cha Novemba hadi Desemba.
Alitoa
utabiri wa msimu wa Oktoba hadi Desemba na kuwataka wakulima wa mikoa ya
Kagera, Geita, Mara, kaskazini mwa Kigoma, Arusha na Kilimanjaro kuendelea na
shughuli zao kama kawaida kwa sababu hali ya unyevunyevu wa ardhi utakuwepo wa
kutosha.
Mkurugenzi
huyo aliyataja maeneo yatakayokuwa na unyevunyevu hafifu wa udongo kuwa ni
Mwanza, Simuyu, Shinyangam Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Unguja, Pemba na
Morogoro.
Akizungumzia
utabiri wa msimu wa kuanzia Oktoba hadi Desemba alisema TMA inawashauri
watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wakiwemo wakulima, wafugaji, mamlaka za
wanyamapori, maji na afya wazingatie utabiri huo na kutafuta ushauri wa
wataalamu wa sekta husika ili kuepuka majanga.
Kwa
mujibu wa Dk. Kijazi utabiri wa mamlaka hiyo kwa msimu uliopita ulifanikiwa kwa
asilimia 88.2 ambapo maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za wastani.






No comments:
Post a Comment