Tazama Liverpool imeshinda 2-0 dhidi ya Olympiakos huku Wayne Rooney nae akicheza huku Man United wakishinda 3-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 04, 2013

Tazama Liverpool imeshinda 2-0 dhidi ya Olympiakos huku Wayne Rooney nae akicheza huku Man United wakishinda 3-0.

Steven Gerrard (kulia) na Joe Allen
wakishangilia baada ya bao la kwanza.
Liverpool  imeshinda 2-0 dhidi ya Olympiakos ya Ugiriki katika mchezo maalum wa kumuaga Nahodha wake, Steven Gerrard baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 15.

Mabao ya Wekundu hao wa Anfield katika mchezo huo yalifungwa na Joe Allen dakika ya 23 na Henderson dakika ya 62.


Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet/Jones dk85 Johnson, Toure/Carragher dk62, Agger, Enrique; Allen/Henderson dk62, Gerrard/Spearing dk85, Lucas, Coutinho/Fowler dk72, Sterling/Alberto dk72 na Aspas/Suarez dk62.


Olympiacos: Megyeri, Maniatis, Fejsa, Mitroglou/Saviola dk56, Samaris/Weiss dk46, Holebas, Medjani/Manolas dk56, Slovas, Siovas, Campbell, Salino na Dominguez.

Jordan Henderson alifunga la pili kwa Liverpool,ikiwa tu ni sekunde 12 baada ya kuingia uwanjani.

Luis Suarez alicheza kwa Liverpool jana(Agosti 03,2013).
Nao wachezaji  Wayne Rooney, Nani, Nemanja Vidic na Javier Hernandez wote walianza kikosini Manchester United katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Real Betis ambao mashabiki hawakuingia Uwanja wa Carrington.

Rooney alicheza dhidi ya Real Betis. 
Mshambuliaji wa England, Rooney alicheza kipindi cha kwanza lakini hakuweza kufunga bao, mabingwa hao wa Ligi Kuu England wakishinda 3-0.

Mchezo huo uliochezwa asubuhi ya jana(Agosti 03,2013) kwenye Uwanja huo wa mazoezi wa United, ulikuwa wa kwanza kwa Rooney baada ya kuumia katika mechi ya kwanza ya ziara ya Mashariki ya Mbali mwezi uliopita.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye hajatulia, amepona maumivu ya nyama za paja aliyoyapata katika ziara ya Asia ya klabu hiyo na jana alionyesha yuko sawa akicheza dhidi ya timu hiyo ya La Liga.

Rooney anatarajiwa kuhama Old Trafford kutimkia Chelsea, ambao ofa yao ya pili ya Pauni Milioni 23 ilipigwa chini.

Anaweza kuwa na mazungumzo zaidi na kocha David Moyes wiki ijayo juu ya mustakabali wake wakati United ikijiandaa kwa mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya AIK mjini Stockholm.

Lakini United inabaki na msimamo wake wa kumbakiza.

Beki Nemanja Vidic akipambana na George Ray wa Crewe Jumatatu. 

Vidic alianza jana (Agosti 03,2013) katika mchezo ambao ulichezwa milango imefungwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad