![]() |
Gonzalo
Higuain akikabiliana na Laurent Koscielny
|
![]() |
Wachezaji
wakiwa wamemzingira refa baada ya Arsenal kupewa penalti, ambayo iliokolewa na
Pepe Reina (wa pili kushoto) baada ya Lukas Podolski kupiga.
|
![]() |
Arsene
Wenger (kulia) akisalimiana na Rafael Benitez (kushoto) kabla ya mechi yao
iliyoisha kwa Arsenal kutoka 2-2 na
Napoli katika Mashindano ya kugombea Emirates Cup .
|
KLABU ya
Arsenal jana ilitoka nyuma kwa mabao mawili na kupata sare ya 2-2 mbele ya timu
ya kocha Rafael Benitez, Napoli katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe lao la
Emirates.
Lorenzo
Insigne na Goran Pandev waliwafungia mabao wageni kipindi cha kwanza, katika
mchezo huo wa kujiandaa na msimu, Gunners wakionekana kuzidiwa kipindi cha
kwanza.
Hata hivyo,
The Gunners walizinduka na kufanikiwa kusawazisha mabao yote, moja la Olivier
Giroud kwa tika tak dakika ya 71 na lingine Laurent Koscielny kwa kichwa dakika
ya 85, baada ya Insigne kufunga dakika ya saba na Pandev dakika ya 29.
Arsenal
walipata nafasi ya kufunga bao la tatu, lakini mkwaju wa penalti wa Lukas
Podolski uliokolewa na kipa Pepe Reina wa Napoli.
EMERATES
CUP 2013.
RATIBA:
[Saa za
Bongo]
Jumamosi
Agosti 3
Galatasaray
Spor Kulübü – Turkey 0 FC Porto – Portugal 1
Arsenal FC –
England 2 Napoli – Italy 2
Jumapili
Agosti 4
15:00 Napoli
– Italy v FC Porto - Portugal
17:20
Arsenal FC – England v Galatasaray Spor Kulübü - Turkey
Katika Mechi
iliyochezwa mapema, FC Porto ilifungwa Bao 1-0 na Galatasaray kwa Bao la
Mbrazil Felipe Melo la Dakika ya 71.
No comments:
Post a Comment