Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kombaini ya Polisi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 04, 2013

Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kombaini ya Polisi.

Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimtoka mchezaji wa Polisi Kombaini, Magige  Machango katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Jana(Agosti 03,2013) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika mchezo huo Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kombaini ya Polisi katika mfululizo wa michezo ya kujiandaa na msimu.


Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Pamba FC ya Mwanza, Betram Mombeki.

Mshambuliaji
wa  Polisi Kombaini, Admin Bantu akimtoka
mshambuliaji wa  Simba, Abdulhalim Humud
katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam

Mshambuliaji wa Simba Betram Mombeki akishangilia goli aliloifungia timu yake dhidi ya Polisi Kombaini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Andrew Ntalla, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Rahim Juma, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Sino Augustino na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.  

Polisi FC; Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon Fanuel, Yahya Khatib, Salmin Kiss, Salum Nahoda, Magige Machango, Andrew Bundala, Mokili Lambo, Bantu Admin na Nicolas Kapibe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad