Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ateua mkuu mpya wa Idara ya Uhamiaji Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 29, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ateua mkuu mpya wa Idara ya Uhamiaji Nchini.


H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete and Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation discussing something during the meeting 33rd SADC Summit.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.

Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza

Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad