H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete and Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation discussing something during the meeting 33rd SADC Summit. |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu
Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
Taarifa
iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti
28, mwaka huu, 2013.
Ndugu
Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi
nyingine.
Kabla ya
uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa
Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza
Rais pia
amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya
Ushirikiano wa Kikanda.
Taarifa
iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28,
mwaka huu, 2013.
Kabla ya
uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za
Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC)
No comments:
Post a Comment