![]() |
Waziri Mkuu wa Bw. Mizengo Pinda. |
Kituo cha
sheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na chama cha wanasheria
Tanganyika kimewasilisha mahakama kuu
jijini Dar-es-Salaam,shauri la mashtaka dhidi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya
mungano wa Tanzania ,Bw. Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema.
Wakiwasilisha
shauri hilo mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam, jopo la mawakili mbalimbali
kutoka kituo cha sheria na haki za binadamum,pamoja na baadhi ya mawakili
kutoka chama cha wanasheria Tanganyika na baadhi ya wanainchi.
Wakiongea na
waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha hati ya mashtaka,mjumbe wa bodi
ya kituo cha sheria na haki za biandamu Dr Ringo Tenga,amesema wanaangali
matamshi yanayo hatarisha haki za biandamu lazima mambo hayo wayafikishe
mahakamani.
Katika hatua
nyingine mwakilishi wa taasisi ya kufuatilia na kuangalia shughuli na mwenendo
wa bunge kwa niaba ya wananchi Bw. Marccosy Albanie amesema kuwa,wanaandaa
mashtaka mengine dhidi ya waziri mkuu kwenda kwa wanainchi,kufuatia kauli yake
kuwa serikali imechoka na hakuna namna nyingine ili wanainchi nao waamue.
Shitaka hilo
litakalo kuwa chini ya mawakili 20,ambapo baada ya kuwasilishwa mahakamani,
kitakachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,
pamoja na jaji atakaye lisikiliza ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa shitaka hilo
kupelekewa walaka wa kuitwa mahakamini ili kujibu mashtaka yanayo wakabili.
Shitaka hilo
namba 24 la mwaka 2013 dhidi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania
mheshimiwa Mizengo na mwanasheria mkuu wa serikali mheshimiwa jaji mstaafu
Fredrick Welema, linafuatia kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni mjini Dodoma
kwenye kikao cha tarehe 20 mwezi wa sita 2013, akiwaamuru polisi kuwapiga wale
wote watakao kaidi kutii amri halali za jeshi la polisi kuwa watapigwa.
No comments:
Post a Comment