Simu zote ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, Mwaka huu. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Wednesday, June 26, 2013

demo-image

Simu zote ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, Mwaka huu.

.com/simgad/


article-2152079-128CB882000005DC-598_306x423

Simu aina ya iPhone5.
Simu zote ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, mwaka huu.




Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema hayo Bungeni jana, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na matumizi mabaya ya simu.



Alisema serikali pia imekamilisha kanuni na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) zitakazodhibiti matumizi mabaya ya simu za mkononi.



“Serikali pia inashirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwasaka na kuwakamata wote wanaotumia simu vibaya,” alisema.




Januari-Makamba
January Makamba.
Makamba alisema Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ilifanya usajili wa namba za watumiaji wa simu za mkononi ambapo hadi sasa namba za simu 24,399,000 zimesajiliwa.



“Usajili wa namba za simu pamoja na masuala mengine, ulikuwa na lengo la kupunguza matumizi mabaya ya simu za mkononi,” alisema.




Makamba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM), ambaye alitaka kujua serikali inasema nini juu ya baadhi ya watu kutumia simu za mkononi kusambaza ujumbe mfupi na maneno ya kuzusha.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *