Taarifa ya
pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za
Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya asilimia
14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazitoweza kukwepesha kupanda kwa gharama
za simu kwa watumiaji.
MOAT inasema
awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu
na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na
Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu
ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
Muswada wa
Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni;
“huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa
njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa
ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia.
”Imesema
taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel, MOAT imesema eneo
mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa
mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na
kijamii na wala sio kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo
kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi
nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki.
“Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume
na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya
msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”
Kwa mujibu
wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma
ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni
asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya
watumiaji asilimia 40.
Aidha, MOAT
imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika
Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao
wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya
MOAT.
Taarifa hiyo
imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35 kwenye sekta
hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza
kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi sasa,
upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta
nzima.
Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu
itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo
wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini,
imesema MOAT.
“Tunaelewa
kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya
kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba
sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa
ongezeko hili.






No comments:
Post a Comment