Taasisi
ya kuhamasisha maendeleo na mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini
Musoma mkoani Mara ya JAMII INFORMATION NETWORK inatarajia kufanya
Kongamano kubwa litakalo wahusisha Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10
za Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya
kuhamasisha Maendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano ndani ya Jamii.
Katika
Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika
Masuala uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya
kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana pamoja na Ukatili wa
Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa Makuzi kwa Vijana wetu.
Mbali
na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi
yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za
uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya
kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
Pamoja
na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado
kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa
katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa
nia njema inakuomba wewe Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya
nchi,Mashirika kusaidia Taasisi hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili
vijana wetu wakue katika Makuzi mema na kujenga Tanzania ya kesho
iliyostaarabika.
Blog
Master
No comments:
Post a Comment