Wanawake DRC
wakiandamana.
|
Shirika la
Save the Children, limeeleza kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa
ndio nchi ngumu zaidi duniani kulea watoto.
Nchi ya
Finland imetajwa kuwa sehemu bora duniani kuwa mama, huku Sweden na Norway
zikifuatia katika nafasi ya pili na tatu.
Shirika hilo
la hisani limetumia vigezo vya huduma ya afya kwa akina mama, vifo vya watoto,
elimu na kipato katika nchi 186 duniani kutoa takwimu hizo.
Nchini
India, zaidi ya watoto 300,000 hufariki dunia saa 24 baada ya kuzaliwa, hivyo
kuchangia 29% ya vifo vya watoto wanaozaliwa duniani kote, imeeleza ripoti ya
shirika hilo.
Nchi kumi
zilizoshika nafasi ya mwisho zote zinatoka eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara,
ambako kwa wastani, mwanamke mmoja katika 30 hufariki dunia kutokana na
matatizo ya ujauzito na mtoto mmoja kati ya saba hufariki kabla ama baada ya
kufikisha umri wa miaka mitano.
Nchini DRC,
vita na umasikini vimewaacha akina mama wakiwa dhoofu kiafya na bila msaada
wowote hasa wakati wa hatari kubwa katika maisha yao.
Nchi
nyingine zilizotajwa kuwa hatari ni Somalia, Sierra Leone, mali, Niger, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Gambia, Nigeria, Chad na Cote D’Ivoire.
Congo
ni mahali hatari zaidi kwa
akina
mama
|
Shirika hilo
la hisani limesema, ukosefu wa lishe bora ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa
idadi ya vifo vya akina mama na watoto wachanga katika nchi za Kusini mwa
Jangwa la Sahara, huku 10% - 20% ya akina mama wakiwa hawana uzito unaostahili.
Kinyume
chake, matokeo hayo yanaonesha kuwa, Finland ni nchi bora kuwa mama, huku
hatari za vifo vitokanavyo na ujauzito ikiwa ni moja kati ya akina mama 12,200
na watoto katika nchi hiyo wakihudhuria karibu miaka yote 17 ya elimu ya awali.
Sweden,
Norway, Iceland na Uholanzi zilikuwa pia miongoni mwa nchi bora 10, ambapo
Marekani iko nyuma katika nafasi ya 30.
Lakini jambo
la kustaajabisha, ripoti ya shirika hilo imebaini kuwa, Marekani ina kiwango
cha juu cha vifo vya watoto wanaozaliwa katika nchi zenye viwanda duniani,
ambapo watoto 11,300 hufariki dunia katika siku wanayozaliwa kila mwaka.
Shirika hilo
limesema, hali hiyo inasababishwa na idadi kubwa ya watu nchini Marekani pamoja
na wingi wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Marekani ni
miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
ikiwa na uwiano wa mtoto mmoja kati ya wanane.
Ripoti hiyo
imegundua kuwa, akina mama na watoto hufariki dunia kwa idadi kubwa huko Kusini
mwa Asia kuliko eneo lolote duniani, ikikadiriwa kuwa, watoto 423,000 hufariki
dunia siku wanayozaliwa kila mwaka.
India
imetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga,(ikiwa ni 29% ya vifo
duniani) na pia vifo vingi vya akina mama kuliko nchi yoyote duniani ambapo
akina mama 56,000 hufariki kila mwaka.
Chanzo:BBC.
No comments:
Post a Comment